Sunday 30 September 2012

Nahodha: Wanaobeza Muungano watimuliwe CCM

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Shamsi Vuai Nahodha amesema viongozi wanaokejeli na kubeza Muungano hawastahili kuendelea kubaki ndani ya chama tawala na serikali zake.
Nahodha alitamka hayo wakati akifungua mkutano wa uchaguzi wa viongozi wanaogombea nafasi mbalimbali ikiwemo ujumbe wa halmashuri Kuu ya Taifa ya CCM NEC wilaya Dimani mjini Unguja jana.
Alisema kimantiki viongozi wanaodiriki na kuthubutu kusimama hadharani bila aibu wakipinga Muungano uliopo amewafananisha na watu waliokosa utu na shukrani.
“Wanaopita na kusema Muungano haufai hata kufika kwao mahali walipo wakipata hadhi na heshima ni kutokana na nguvu za CCM na serikali zake,” alisema Nahodha.
Aliwafananisha watu hao na wasaliti wanaotoboa jahazi wanamosafiria huku wakiwa kwenye kina kikubwa cha bahari.
Nahodha ambaye ni Waziri Kiongozi mstaafu wa SMZ alisema yuko tayari kupoteza marafiki kwa na kubaki kuwa mtetezi na muumini wa Muunagno wa serikali mbili.
“Sitajutia kupoteza marafiki wanafiki katika mambo ya msingi yanayogusa umoja wa kitaifa, potelea mbali liwalo na liwe,” alisema Nahodha.
Akizungumza na kuufanya ukumbi kukaa kimya, Nahodha aliwataka viongozi wenye fikra mbadala kupitisha mawazo yao kwenye vikao vya kikatiba na wakishindwa watoke kama hawakubaliani na misimamo ya kisera ya chama hicho.
Alisema siri ya Muungano huo chini ya waasisi wake hayati Baba wa Taifa na Sheikh Abeid Karume ni dhahiri walizingatia na kuweka mbele maslahi ya umoja kwa kupinga utengano.
Akizungumzia umuhimu wa kuwachagua viongozi bora kwa miaka mingine mitano ijayo wanachama wenzake kuchagua wenye sifa za uadilifu, uaminifu na majasiri katika kutii sera za chama na kuheshimu katiba yao.
“Huu si wakati wa kuchagua viongozi kwa pupa na papara, chagueni kwa umakini, msichague viongozi mamluki wanaojibadili rangi zao kuliko kinyonga na kuhatarisha uhai wa chama chetu,” alisema Nahodha.
Kauli hiyo ya Nahodha imekuja huku baadhi ya makada na viongozi wa juu wa CCM Zanzibar wakipigania kuwepo kwa Muungano wa mkataba agenda ambayo pia inapigiwa upatu na Jumuiya ya kidini ya Uamsho visiwani humu.
Hata hiyo viongozi hao wamekumbana na upinzani mkali toka kwa waaasisi wa Mapindzi na Muungano ambao wanapinga vikali wazo la Muungano wa mkataba wakiamini mpango huo umebeba ajenda ya siri ya kuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Uchaguzi CCM: Majonzi yatawala vigogo Zanzibar

Uchaguzi wa CCM Zanzibar ilifanyika jana huku ukiacha majonzi kwa wanasiasa maarufu, akiwemo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Khamis Suleiman Dadi, wakianguka.

Mwanasiasa huyo maarufu katika siasa za Zanzibar aliagushwa na wagombea wenzake katika nafasi ya NEC kupitia Wilaya ya Chake Chake Kisiwani Pemba.

Vigogo wengine walioanguka Wilaya ya Mjini ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Mohamoud Thabiti Kombo; Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo, Nassor Salim Ali; Mbunge wa Jango’mbe, Hassan Mussa Mzee; aliyekuwa Mbunge wa Kikwajuni, Paramuk Singa Hogani, na kadawa chama hicho, Baraka Mohamed Shamte.

Wengine katika Wilaya ya Kati Unguja ni aliyekuwa Waziri wa Maji Ujenzi Nishati na Ardhi, Tafana Kassim Mzee na aliyekuwa Mbunge wa Mpendae, Issa Kassim Issa.

Vigogo wengine waliopiga mweleka ni Naibu Waziri wa Afya, Dk. Sira Ubwa Mamboya, ambaye aligombea kupitia Wilaya ya Dimani, wakati Naibu Spika Ali, Abdalla Ali, alianguka kupitia Wilaya ya Mfenesini.

Walioibuka kidedea katika katika Wilaya ya Chake Chake nafasi ya Mwenyekiti ni Kombo Ali Kombo. Wajumbe wa NEC ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza Mohamed Aboud Mohamed; Ali Issa Ali, Seif Shaaban Mohamed, Mbarak Said Rashid, Hamad Bakary Ali na Suleiman Farahan Said.

Wilaya ya Kati nafasi ya uenyekiti aliyeshinda ni Hassan Mrisho Vuai. Wajumbe NEC ni Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, Ramadhan Abdalla Shaaban; Balozi Ali Karume, Asha Mshimba Jecha, Khalfan Salum Suleiman, Kombo Hassan Juma na Haji Mkema Haji.

Wilaya ya Wete Mwenyekiti ni Kombo Hamad Yussuf na Wajumbe wa NEC ni Maida Hamad Abdalla, Maua Abeid Daftari, Asiya Sharif Omar, Makame Said Juma, na Hamad Faki Juma.

Wilaya ya Amani Mwenyekiti ni Abdi Ali Mzee, Wajumbe wa NEC Vuai Ali Vuai, ambaye pia Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Juma Khamis Haji, Situmai Mohammed Msimbe, Muhamad Amour Chombo, Rashid Ali Juma ambaye ni Mkurugenzi wa Manispaa ya mji wa Zanzibar na Nadra Juma Mohamed.

Wilaya ya mjini Mwenyekiti ni Juma Faki wakati wajumbe wa NEC ni Hamad Yussuf Masauni, Burhani Saadati Haji, Asha Abdalla Juma, Talib Ali Talib, Sufiani Khamis Ramadhani na Omar Jastus Morris.

Wilaya ya Kaskazini A Menyekiti Ali Makame Dilunga na wajumbe wake NEC ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi wa Umma na Utawala Bora), Haji Omar Kheir, Ali Juma Chepe, Ussi Yahya Haji, Ame Mati Wadi, Mussa Ame Silima na Khamis Mohamed Mahamoud.

Wilaya ya Kaskazin B Mwenyekiti ni Hilika Fadhir Khamis na wajumbe ni Abeid Mohamed Khamis, Mtumwa Pea Yssuf, Bahati Ali Abeid, Miraji Khamis Mussa, Abdulhamid Hassan Juma na Bhati Ali Abeid.

Katibu Mwenezi wa CCM Zanzibar, Issa Haji Gavu, alisema matokeo ya uchaguzi wa Wilaya zote 12 za Zanzibar wanatarajia kutangaza leo.

Chanzo: Nipashe

Watanzania waache uchama watafute mifumo mingine

Mzalendo Ahmed Rajab
WALIOLEWA kasumba ya ubepari watayakebehi haya niyaandikayo na hawatoyaamini kamwe lakini ukweli uliopo ni kwamba mfumo wa kiuchumi wa kibepari umekwisha zake.
Hiyo si ndoto tu ya muumini wa mfumo mbadala wa kiuchumi wenye kujengeka juu ya misingi ya haki, usawa na unaopinga unyonyaji wa aina yoyote hasa wa wachache kuwanyonya walio wengi, lakini ni hitimisho la wataalamu mbalimbali walioitalii historia ya mfumo huu wa kibepari, mfumo wenye umri wa takriban karne sita tangu ulipoanza kushamiri mwaka 1500 hadi sasa mwaka 2012.
Kwa mujibu wa wataalamu hao kipindi hiki tulicho nacho sasa ni kipindi cha mwanzo wa mwisho wa kusambaratika kwa ubepari ukiwa ni mfumo wa kiuchumi wa dunia. Wanachosema wataalamu hao ni kwamba kipindi hiki tulicho nacho kinaashiria mauti ya mfumo wa ubepari kama tuujuavyo.
Miongoni mwa wataalamu hao wanaojulikana sana na wasomi wa Tanzania, hasa wale wenye mwelekeo wa mrengo wa kushoto ni Immanuel Wallerstein, mwanasosiolojia wa Kimarekani mwenye umri wa miaka 81 na ambaye pia ni mchambuzi wa mifumo ya dunia.
Wengine ni mtaalamu wa mambo ya uchumi mzaliwa wa Misri Samir Amin mwenye umri wa miaka 80 na mwanasosiolojia wa Kitaliana Giovanni Arrighi aliyefariki dunia mwaka 2009 na aliyewahi kufundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako ndiko alikokutana na Wallerstein.
Hao na wenzao, wote wakiwa wafuasi wa nadharia ya Umarx, wamekuwa wakiutalii na kuufanyia utafiti mfumo wa ubepari wa dunia tangu miaka ya 1960. Baadaye wakaugeukia utandawazi na wamekuwa wakiufanyia utafiti mwingi hasa baada ya kuporomoka kwa Muungano wa Kisovieti na kuchomoza kwa Marekani kuwa ndiyo dola kuu pekee duniani.
Utafiti wao pamoja na wa wachambuzi wengine, baadhi yao ambao si wa mrengo wa kushoto, unaonyesha wazi jinsi mfumo wa ubepari unavyovuta pumzi zake za mwisho.
Hivi majuzi nilikuwa nikisoma mahojiano aliyofanyiwa Paul Craig Roberts, aliyewahi kuwa waziri mdogo wa hazina katika utawala wa Rais Ronald Reagan huko Marekani.
Roberts, ambaye pia ni mtaalamu wa mambo ya uchumi, alihojiwa na mhariri wa jarida moja liitwalo Torture Magazine. Katika mahojiano hayo hata yeye Roberts alikiri kwamba ubepari wa Kimarekani uko taabani.
Sababu kubwa alizozitaja Roberts za kudhoofika kwa mfumo huo ni mbili. Kwanza, kuvunjika kwa Muungano wa Kisovieti na pili kuibuka kwa mtandao wa mawasiliano wa intaneti ambao ulichangia pakubwa katika kuuimarisha utandawazi.
Matokeo ya kuimarika kwa utandawazi ni kwamba uliwezesha uzalishaji wa bidhaa kwa masoko ya Marekani uhamishiwe katika nchi za nje ambako mishahara ya wafanya kazi viwandani ni midogo kulinganishwa na ile ya Marekani kwenyewe.
Kudhoofika kwa uchumi wa Marekani na sokomoko linalozikumba chumi nyingine za nchi kadhaa za Ulaya ni ishara moja tu inayoonyesha kuwa kuna msukosuko mkubwa utaoukabili mfumo wa ubepari katika miaka ya karibu. Msukosuko huo ndio utaoumaliza kabisa huu mfumo tuliouzoea wa ubepari wenye kuongozwa na Marekani na mataifa mengine ya Magharibi.
Kila mfumo — nauwe adhimu namna gani — lazima iko siku utaoza na kusawijika. Barani Afrika tumeona jinsi umwinyi ulivyokufa, jinsi tawala za kidikteta zinavyotoweka na jinsi baadhi ya tamaduni za Kiafrika zinavyoachwa mkono kwa vile zinakwenda kinyume na nyakati tulizo nazo. Si tamaduni zote za Kiafrika zinazoachwa mkono ni baadhi tu; nyingine zimo hatarini kwa vile zinaingiliwa na kupigwa vita na utamaduni wenye kutawala duniani.
Hata huu mfumo wa usasa (modernity) ulioanzia barani Ulaya nao pia hautonusurika. Utaishia kulekule zilikoishia taratibu nyingine za kiuchumi, kisiasa na kitamaduni.
Mfumo wa usasa ni mfumo uliozaliwa barani Ulaya. Kwa hakika mfumo huo ulianzia ndipo yaani kwa misingi mizuri. Ulianza kwa kuwa mfumo wa kimaendeleo uliokuwa na mvuto wa aina yake (ingawa nyakati nyingine ulionyesha kuwa wa kilaghai).
Usasa ulikuwa ni aina ya mapinduzi kwani mfumo huo ulianzisha vuguvugu lililokwenda kinyume na mamlaka ya Kanisa. Vuguvugu hilo pia lilikuwa dhidi ya miiko ya kidini, lilipinga ugandamizaji wa kidini, lilipinga ‘inquisition’ ule msako wa kanisa Katoliki wa kuwafichua waasi na kuukomesha uasi dhidi ya mafundisho asilia ya kanisa hilo. Kadhalika, vuguvugu lilipinga ile tabia iliyoshtadi siku hizo miongoni mwa Wakatoliki ya kuwachoma moto wale waliokuwa wakidhaniwa au kusingiziwa kuwa ni wachawi.
Kwa ufupi, usasa ulipoingia mjini uliingia mjini ukisherehekea maisha, ukiadhimisha elimu na maarifa, ubinafsi, uhuru, na haki za binadamu. Hivyo usasa ulimfanya mwanadamu awe na moyo mpya uliomfanya awe na ari ya kufanya ugunduzi wa kisayansi, kuendesha biashara baina ya watu na baina ya mataifa kwa njia za kisasa, na pia usasa uliwezesha kupatikana mchipuko wa kisanaa uliokuwa wa kifahari na uliojawa taadhima kubwa.
Lakini katika wakati huu tulio nao usasa umepoteza haiba yake ya awali. Badala ya kuwa alama ya uhuru, uadilifu na haki za binadamu umegeuka na kuwa alama ya ushindi wa nchi moja kuiteka nyingine, ukoloni, ugandamizaji na uangamizwaji wa mazingira. Usasa umekuwa ukienda sambamba na kushirikiana na ubepari.
Ubepari nao ulipoingia mjini na kuung’oa ule mfumo wa umwinyi ulikuja na mvuto wake pia. Ingawa barani Afrika mfumo huo wa ubepari ulichelewa kufika hata hivyo hivi sasa umeingia kwa nguvu. Na si Afrika tu lakini pia katika sehemu nyingine za dunia ambazo hazikuweza kujiendeleza kwa sababu ziligand amizwa na wakoloni pamoja na mabeberu.
Kwa hakika, ubepari tangu ulipofungua macho miaka hiyo 600 iliyopita hadi leo umeweza kujizatiti kuenea dunia nzima na umekuwa ushawishi mkubwa katika nyanja mbili muhimu: za siasa na utamaduni. Katika upande w a siasa tunaona jinsi demokrasia ya kilib erali inavyoutumikia na kuuhami mfumo uliopo wa kibepari. Mfumo huo eti unaitwa ‘ubepari wa kidemokrasia’ ili kutufanya tuamini kwamba una haki na usawa.
Tukiugeukia utamaduni uliotTukiugeukia utamaduni uliot Tukiugeukia utamaduni uliot ia fora duniani hii leo tunaona kuwa huo ni utamaduni ulioathiriwa kwa kiwango kikubwa mno na ubepari. Unaweza hata kusema kwamba utamaduni huo kwa kweli umezaliwa na ubepari hasa ule ubepari wa Kimarekani ambao ndio wenye kuongoza duniani.
Angalia jinsi utamaduni huo ulivyoweza kupen ya na kukubalika hata katika jamii kama ya China iliyokuwa kwa miongo kadhaa ngome ya kupinga tashwishi za kitamaduni kutoka nchi za nje hususan zile Magharibi zilizo za kibepari.
Utamaduni huo wa Kimarekani unatumiwa kuuendeleza huo mfumo wa kibepari na kwa vile utamaduni huo ndio wenye nguvu na kudirizi basi tamaduni zetu za Kiafrika zimo hatarini.
Zinashambuliwa kila upande kwa mishare ya kila aina na tanzu zake zote hii leo zimo zikijikokota zikijaribu kuhepa zisije zikamezwa na huo utama duni wenye kuitawala dunia.
Kuna uongo mwingi uliokuwa ukisemwa miaka nenda rudi na wataalamu wa kiuchumi wenye kuutetea mfumo wa kibepari. Moja ya uongo huo ni ule usemao kwamba katika mfumo wa kibepari yeyote anayefanya kazi kwa bidii anaweza kuw a tajiri.
Uongo mwingine, na p engine mkubwa kushinda yote, ni kwamba ubepari unazalisha utajiri na ufanisi kwa wote katika jamii.
Kuna p ia uzushi kwamba jamii ya kibepari haina matabaka, kwamba watu walio ndani ya jamii hiyo wanawajibika sawa na wengin e. Kinachosemwa hapa ni kwamba tuseme kwa mfano kuna hali mbaya ya uchumi kama ilivyo sasa katika nchi za Magharibi basi wafanyakazi na matajiri wote wana dhima sawa.
Uzushi mwingine ni kwamba ubepari unaleta uhuru, demokrasia na kwamba njia ya ku fikia demokrasia ni kupitia ile ya chaguzi za kila baada ya kipindi cha miaka fulani. Watetezi wa mfumo kibepari aghalabu hawachelei kukiri kwamba kweli ubepari una madosari yake lakini hapohapo hushikilia kwamba huo ndio mfumo pekee wa kiuchumi na kis iasa uliopo na hivyo ndio mfumo unaofaa kufuatwa kwa vile hakuna mfumo mbadala.
Kwa kusema hivyo watetezi hao wa ubepari wanakuwa wanaepusha pasifanywe mijadala ya kuangalia ni mifumo gani mbadala inayoweza kufuatwa minghairi ya ule wa ubepari.
Labda huu mchakato unaoendelea wa kulitafutia Taifa katiba mpya ni fursa aifa katiba mpya ni fursa nzuri kwa Watanzania kutafakari ni mfumo gani wa kiuchumi na kisiasa wawe nao licha ya kwamba wana vyama tofauti vya kisiasa. Ingawa vyama hivyo ni tofauti lakini kimsingi havina tofauti kubwa kwani vyote vinahubiri aina ya ubepari.
Mfumo huu wa ubepari hautufai. Kwanza kwa sababu unakufa na tumekwishashuhudia madhara yake kwa jamii zilizoendelea kiuchumi kushinda hii yetu.
Pili , kwa sababu humuhumu ndani nchini tunashuhudia kila uchao jin si mfumo huo unavyoulea ufisadi, jinsi unavyotumiwa na tabaka la wanasiasa kuzidi kujijenga na kujinufaisha na huku idadi ya walalahoi ikizidi kuongezeka na maisha yao yakizidi kudidimia.
Mfumo huu umekuwa kama mchwa — unaila hasa nafsi ya Afrika.
Chanzo: Raia Mwema

Zanzibar plagued by growing heroin addiction

 Residents say it is relatively easy to smuggle the drug on and off the East African island

There are an estimated 9,000 heroin addicts on the small East African island of Zanzibar - one of the highest rates of usage in the world.
Zanzibar’s container port is along several key shipping routes that ferry the drug from Asia to big markets in the US and Europe.
And residents say it is relatively easy to smuggle heroin on and off the island.
Although the drug is illegal in Zanzibar, it is almost impossible for the authorities to know what goods are coming or going.