Thursday 29 November 2012

Karume “mpuuzi”, lakini ukweli wake mchungu

MAKALA hii itahitimisha tathmini yangu kuhusu Mkutano Mkuu wa 8 wa CCM uliofanyika Dodoma tangu Novemba 11 hadi Novemba 14 mwaka huu.
Kwa kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) ni chama dola, vimbwanga vyake huwa vinachanganya watu na kuamini kuwa kila baada ya Mkutano Mkuu, CCM huwa inazaliwa upya.
Imani hii imejengeka kutokana na ukweli kuwa, kabla ya Mkutano Mkuu, huwa kuna dalili za migawanyiko na mipango kadhaa ya makundi kutaka agenda zao zishinde.
Kutokana na udhibiti wa vyombo vya dola pamoja na ushabiki uliopitiliza, mipango hiyo huwa inakwama na kuwafanya watu wengi kuamini kuwa CCM ina wenyewe, na wenyewe hao huwa wanaifanya izaliwe upya kila baada ya Mkutano Mkuu!
Historia ya dhana hii ni ndefu, na wahanga (victims) wa mkakati huu kwa miaka ya karibuni ni Salmin Amour (Komandoo), Mzee John Malecela, Dk. Gharib Bilal, Samuel Sitta na sasa Edward Lowassa.
Kwa miaka ya nyuma wanakumbukwa Mzee Aboud Jumbe na Sharrif Hamad. Kwa sababu zilizo wazi, mkakati huu wa kuipa uhai mpya CCM huwa unawaathiri sana Wazanzibari kuliko Watanganyika.
Rais Karume na “upuuzi” wake
Kama Makamu Mwenyekiti anayemaliza muda wake, rais mstaafu Amani Karume alikaribishwa kutoa nasaha zake siku ya kufunga mkutano. Alitoa hotuba, ambayo hivi sasa inaitwa ya kipuuzi huko Magogoni na mtaa wa Lumumba.
Hakuna aliyetarajia kuwa Karume angesema maneno aliyoyasema siku hiyo kiasi cha Mwenyekiti Jakaya Kikwete kukiri kuwa “hajawahi kumwona amefurahi kiasi hicho” kama alivyomwona siku hiyo.
Mara kadhaa hotuba yake ilikatishwa na watu waliomzomea na kumtaka amalize na kukaa. Hii ikakumbusha enzi za uenyekiti wa Benjamin Mkapa wakati wanamtandao wa Kikwete walipokuwa wakimzomea kila mtu aliyetaka kuhoji matumizi ya rushwa katika mkutano huo.
Mzee Joseph Butiku anaikumbuka hii na aliiandikia barua rasmi kwa Mwenyekiti Mkapa. Hii itukumbushe kuwa zomea zomea haikuanza na CHADEMA katika mikutano.
Alipozomewa sana, Rais Karume akawafananisha wazomeaji na vinywa vya samaki! Wapo waliodai, Rais Karume alikuwa kalewa sana konyagi siku hiyo. Awe alilewa au hakulewa; ni mpuuzi au si mpuuzi; kwangu mimi si habari. Habari muhimu ni yale aliyoyasema kwa dakika alizopewa.
Karume alizungumzia kadi yake ya ASP (Afro Shiraz Party); akaelezea madhumuni ya ASP; akamwuliza Dk. Shein ikiwa yeye anayo kadi yake ya ASP. Moja ya madhumuni ya ASP akakumbusha kuwa ni kulinda uhuru wa Zanzibar na watu wake. Ndipo akahoji wale wanaowazuia wenzao wasitoe maoni yao kuhusu Muungano.
Akamkumbusha Rais Kikwete kuwa alitoa ruhusa kila mtu aseme anachotaka wakati wa mchakato wa kutoa maoni ya katiba mpya. Akahoji iweje sasa wengine wanakamatwa kwa kutoa maoni yao. Karume akakumbusha jinsi CCM ilivyopoteza baadhi ya majimbo kwa sababu ya kupuuzia maoni ya wananchi. Akakumbusha suala la zamu kati ya mbunge na mwakilishi katika jimbo fulani. Wazomeaji hawakutaka kusikia haya wakamwimbia taarabu ya “uamsho uamsho”.
Niseme wazi hata kama nilichoka nikakaa nje ya ukumbi wakati anaongea, Karume alisema mambo ya maana kuliko hotuba za masaa zilizotolewa na waheshimiwa wengine. Kwa muda mfupi, Karume aliuzodoa udikteta unaoabudiwa ndani ya CCM; alibainisha hatari zinazoukabili Muungano; alikumbusha habari za zamu za kuongoza nchi hii iliyotokana na nchi mbili; na zaidi sana alisema kutoka moyoni kuwa ASP haijafa kwa sababu waliokuwa wanachama wake wangali bado hai. CCM tumeze au tuteme, huo ndio ukweli kutoka kwa Karume, ambao sasa unaitwa ni upuuzi na akina Nape Nnauye.
Kulialia na kulalama kulizidi mno
Kwa siku tatu, Watanzania walishuhudia wajumbe zaidi ya 2000 wakilialia na kulalamika ndani ya ukumbi. Mwenyekiti alizindua uliaji huo na kupokewa na wajumbe kwenye vikao visivyo rasmi katika nyumba za kulala wageni na kwenye magari. Kivuli cha Chama cha Denokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiliwatesa sana wajumbe na kuwafanya viongozi kupoteza mwelekeo na kuanza kutukana ovyo ovyo.
Haikutarajiwa kuwa Mwenyekiti naye angeingia katika mtego huo, pale alipojikuta anawatukana wapinzani na hasa CHADEMA kwa kuwaita “watu wazima ovyo”, au pale ndani ya NEC alipojikuta anatumia muda mwingi kumpamba Nape Nnauye kwa kuwa anajua kutukanana na CHADEMA. Hata pale alipokumbushwa na rafiki yake kuwa kuitukana CHADEMA si lazima kuijenge CCM, yeye aliishia kusema “wamezidi acha Nape awashughulikie”. Kazi inayomshinda yeye, anaona ni bora aifanye Nape. Kama Mzee Rashidi Kawawa alivyokuwa kwa Mwalimu, Nape ndivyo kwa Kikwete!
Mzee mkorofi kutoka Nyanda za Kusini alihoji, inakuwaje CHADEMA iwe tishio kwa CCM kuliko ufisadi na rushwa ulivyo tishio? CHADEMA inakuwaje tishio kuliko “unduguneizesheni” unaotafutiwa nafasi ya kutambuliwa kwenye katiba ya chama chetu?
Akasema, inakuwaje washauri wakuu wa Mwenyekiti wa chama chetu kuhusu masuala ya chama, si vikao bali ni wanausalama waliojaa fitina? Huyu naye alikuwa analalama sawa tu na wengi waliokuwa wanalalamika kwa siku tatu za mkutano.
Membe: Alimzamisha Mangula; Amemuibua tena.
Nafasi ya Bernard Membe kwa siasa za taifa hili kwa siku za usoni ilikuwa katika mtihani mgumu sana. Kambi ya rafiki yake wa zamani Edward Lowassa ilipania kumzamisha lakini akaokolewa na Kikwete na familia yake.
Kikwete alimsaidia kwa kubadili ratiba za upigaji kura, wakati familia yake (mkewe na mtoto wake) walihaha kila kona kumtafutia kura Bernard Membe. Taifa hili siku moja litadai kujua ukweli wa uhasama na urafiki wa watu hawa watatu – Membe, Kikwete na Lowassa. Jina Kikwete limekaa katikati kwa makusudi. Yeye ni ufunguo wa kitendawili hiki. Hili tuliache kwa sasa.
Mzee Philip Mangula, akaibuka ghafla kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara. Ni huyu huyu ambaye kundi la mtandao lililomwingiza Ikulu Kikwete lilidai alilitesa sana wakati wa kampeini na kuamua kumtosa mara baada ya Kikwete kuapishwa.
Yasemekana, Benard Membe, kachero mzoefu na kiini cha mikakati ya wana mtandao asilia, alimwambia Kikwete kuwa Mangula aliwapa taabu sana hivyo aondolewe kwenye nafasi ya ukatibu mkuu wa chama. Haikuishia hapo, Mzee Mangula alipojaribu kuibukia Iringa kama Mwenyekiti wa Mkoa alishughulikiwa vikali na kuangushwa na mtu asiyefanana na CCM kwa vigezo vyote.
Mzee Mangula alikiri baadaye kuwa ndani ya CCM uongozi uko mnadani na wapiga kura hawataki tena vipeperushi vya wagombea, bali wanataka “vipeperushwa”. Mzee Mangula, kila anapokumbushwa harakati za wana mtandao, huwa anatania kuwa yeye aliponzwa na “faili maalumu”.
Kuna habari kuwa Mzee Mangula kaibuka kwa mkono wa Membe. Kwamba, vikao kadhaa vilifanyika Makambako kati ya wawili hawa. Iwe kwa Membe kujituma au kutumwa, ni kwamba walikutana na agenda ilikuwa ni uchaguzi katika Mkutano Mkuu wa 8.
Aliombwa radhi au hakuombwa, hilo sasa si habari. Habari ni kuwa, Mkutano Mkuu umempitisha Mzee Mangula kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM lakini mshenga mkuu alikuwa Membe. Kama ushenga huu ulikuwa ni kwa manufaa ya chama au kwa manufaa ya mtandao wake anaouunda kwa ajili ya 2015, ni suala la wakati.
Ikiwa ni kweli, basi itakuwa vigumu kukemea mitandao ndani ya chama hiki kikongwe. Kama mtandao wa Membe ni halali, wa Lowassa hauwezi kuwa haramu. Kama Kikwete aliingia kwa mtandao, ni vigumu kuifikiria CCM na urais bila mtandao. Na tumejifunza kwa uchungu kuwa mtandao hauishii katika uchaguzi kwa sababu, baada ya mtu wao kuchaguliwa, kinachofuata ni kufaidi jasho na matunda ya kazi.
Kwa walioshindwa, kuna kazi ya kutathmini ni wapi wamekwama na kuazimia aluta continua. Ni ndoto kuambiana kuvunja makundi wakati anayeshinda na kuingia Ikulu anaendelea na kundi lake.
Jambo moja tu Mzee Mangula alizingatie. Membe anayedaiwa kumzamisha baada ya uchaguzi wa mwaka 2005 mbele ya Kikwete, hawezi kugeuka leo na kumtetea kuwa ni mtu mzuri anayekifaa chama. Kwa nini hakufaa mwaka 2005 chini ya Mwenyekiti huyuhuyu? Membe ni yule yule, Mwenyekiti ni yule yule, chama ni kile kile na Mangula ni yule yule! Ni kitu gani kimebadilika kumfanya Mangula asiyefaa mwaka 2005, afae mwaka 2012?
Kinachoonekana lakini hakizumguziwi waziwazi, ni ukweli kuwa Kikwete na Membe wanamwona swahiba/hasimu wao Lowassa kuwa sasa ni zaidi ya mgombea urais wa CCM 2015. Kwao, Lowassa amegeuka kuwa chama; ameiteka CCM mbele ya macho yao na wanadhani Mangula atawasaidia kuiokomboa CCM iliyo mateka mikononi mwa Lowassa. Kikwete na Membe hawajiulizi ni kitu gani kimemjenga Lowassa na kumfanya kuiteka CCM.
Kitendo cha kumkimbilia aliyekuwa “adui” yao na chama chao kuwa aje kuwasaidia kukijenga chama walichokibomoa kwa mikono yao, hakieleweki. Wengi tulidhani, Mkutano Mkuu ungepata nafasi ya kutathmini hali hii, badala yake tukaambulia kulialia na vijembe visivyo na mpangilio. Tusubiri Mkutano Mkuu mwingine maalumu au ule wa 2017.
Chanzo: Raia Mwema

Tuesday 27 November 2012

Siasa isiingilie uhuru wa Mahakama Z’bar

Na Salim Said Salim
TUNAAMBIWA kuwa hapa nyumbani na nje katika mfumo wa utawala bora wa haki na sheria dhamana kwa mshitakiwa ni haki, japokuwa mahakama ndiyo yenye uamuzi wa mwisho juu ya suala hili.
Nchi nyingi zenye utawala wa demokrasia zimeweka utaratibu unaojaribu kwa kiasi fulani kuhakikisha mahakama hazitumii vibaya mamlaka yake katika suala la dhamana.
Hii ni kwa sababu ipo dhana yenye nguvu inayosema kumuwekea mshitakiwa masharti magumu ya dhamana yanatoa tafsiri ya kuwa sawa na kumnyima dhamana au kuanza kumuadhibu mtuhata kabla hajatiwa hatiani.
Katika baadhi ya kesi zinazoendelea Zanzibar hivi, hasa zile zenye harufu ya kisiasa, kuchimba almasi au dhahabu ni rahisi kuliko kupata dhamana.
Hali hii imesababisha baadhi ya watu,Visiwani na nje, kuuliza kwa kiasi gani mahakama za Zanzibar zipo huru?
Mimi ukiniuliza jibu langu ni kwamba nasikia kuwa zipo huru, lakini sizioni kuwa huru.
Baadhi ya watu Visiwani, hasa wanasheria, wanasema panapokuwepo kesi zenye mashiko ya kisiasa ya aina moja au nyingine mahakama za Zanzibar huwa zinendeshwa kwa kitufe cha mbali (remote control).
Maelezo haya yamepata nguvu kutokana na mahakimu na majaji kueleza mara nyingi kuwa wamekuwa wakipewa amri na wakubwa, baadhi ya wakati kwa kutumiwa vikaratasi, juu ya namna wanavyotakiwa kuendesha kesi.
Unapokuwa na mtindo wa aina hii, hata ikiwa kwa kesi chache sana, basi majumuisho unayopata ni kuwa mahakama hazipo huru na kwamba zimegeuzwa kuwa sehemu ya utawala badala ya kuwa eneo lililo huru na linalotoa na kulinda haki.
Mahakama za Zanzibar hivi sasa zimekuwa zikitoa masharti ya dhamana ambayo unaweza kusema magumu sana au hayatekelezeki na hali hii imezusha wasi wasi juu ya huo uhuru wa mahakama unazungumzwa.
Zanzibar imekuwa na sifa ya kuweka masharti magumu ya mtuhumiwa kupewa dhamana na baadhi ya masharti haya ni ya aina yake na ya kipekee ambayo husikii kuwekwa Tanzania Bara au katika nchi yoyote ile inayojinadi kuwa na mazingira ya utawala wa haki na sheria.
Baadhi ya masharti haya, kama nilivyoeleza siku za nyuma, yana sura chafu ya kuwabagua raia na kuwaweka katika madaraja mawili, moja la watukufu na lingine ni la watu ambao mahakama haitaki kuwaamini. Hawa watukufu ni wale wanaofanya kazi serikalini na wasiostahiki kuaminiwa na kuheshimiwa ni wale ambao sio wafanyakazi wa serikali.
Siku hizi imekuwa kawaida kusikia mshitakiwa anaambiwa kwamba wadhamini wake lazima wawe watumishi wa serikali wakati inajulikana wazi kuwa mtumishi wa serikali hawezi kuhatarisha ajira yake kwa kukubali kuwa mdhamini katika kesi ambayo watuhumiwa wake wamekuwa wakizungumzwa na viongozi wakuu wa nchi.
Mfano mmoja ni wa kesi inayowakabili viongozi wa jumuiya ya Kiislamu ya Uamsho. Hivi mfanyakazi gani wa serikali atajitokeza kuwawekea dhamana?
Tusidanganyane, huu sio mchezo mzuri na ndio maana wananchi wengi na hata hao tunaowaita washirika wetu wa maendeleo wanauona hauonyeshi haki kutendeka.
Au vipi kijana ambaye hana hata kiwanja utamtaka aweke dhamana waraka wa nyumba wakati hata hivyo viwanja hugawiana wakubwa na watu wanaohusika na ugawaji hujigawia wao, watoto, wake zao na hata wajukuu? (angalia ripoti ya tume ya uchunguzi juu ya ugawaji wa viwanja).
Kama majina ya kweli na sio ya bandia ya watu waliopewa viwanja yatawekwa hadharani utaona watu hoe hae kama akina Salim Said Salim ambao hawapo tayari kuwaabudu viongozi kwa ajili ya kutaka vyeo au kulinda urafiki hutayaona.
Majina ya waliopewa viwanja yatawekwa hadharani. Sasa vipi mtu masikini utamtaka aweke kaburi la mzee wake.
Jamani zama za kuifanya Zanzibar kuwa na haki ya kufanya tutakalo, licha ya kutia saini mikataba ya kimataifa ya kuheshimu haki za binaadamu, ikiwa pamoja na za washitakiwa, zimepita. Siku hizi nchi haziruhusiwi na hzivumiliwi ukiukaji wa haki za binaadamu au za washitakiwa.
Mtindo huu wa kuwabagua watu wa Zanzibar kwa mafungu ni wa hatari na utaiathiri Zanzibar. Fikiria serikali itahisi vipi kama watatokea watu na kusema wanaoruhusiwa kuingia katika hoteli au maduka wanayoyamiliki ni wale tu ambao sio watumishi wa serikali?
Kama serikali kupitia mahakama, ina wabagua watu kwanini na wananchi nao wasiwe na haki ya kuendeleza sera hii ya ubaguzi kwa kutumia mali zao?
Lakini kama serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar inataka kurejea tulikotoka ambapo kulikuwepo mahakama za wananchi (mahakimu wazee wanaosinzia hovyo) na kutojali uhuru wa mtu na hata kutoa hukumu kabla ya kesi kusikilizwa basi serikali isione aibu kutamka hivyo.
Kinachosikitisha ni kuona haya yanafanyika wakati Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na ile ya Mkurugenzi wa Mashitaka inaongozwa na watu wenye kuheshimika katika fani ya sheria, lakini wamekaa kimya kama vile kutoa masharti magumu au kumnyima mshitakiwa dhamana ni jambo zuri na linalofaa kupongezwa.
Nilitegemea wanasheria wenye kuheshimika kama hawa wawili wanaoongoza taasisi hizi muhimu za serikali, wangejitokeza kupinga mwenendo huu wa kibaguzi, lakini inaonekana wameweka maslahi yao mbele kuliko yale ya kulinda haki na sheria.
Wazanzibari waache utamaduni wa kulindana kwa maovu. Watu anaojiita waungwana hulindana kwa mambo mazuri na sio mabaya, hasa yale yanayoitia nchi dosari. Lakini hata jumuiya za kiraia zimekaa kimya, labda kwa kuhofia msajili kuzifuta, lakini ukweli lazima usemwe, potelea mbali liwalo na liwe.
Wazanzibari wanataka kuwa na utawala wa haki na sheria za kweli na sio bandia kama inavyojitokeza sasa.
Wazanzibari wengi walikuwa na imani na matumaini makubwa na serikali ya umoja wa kitaifa katika kusimamia haki na sheria, lakini kinachoonekana hivi sasa ni kwamba ndoto yao haikuwa ya asubuhi, mchana wala usiku.
Hakuna kitu kibaya katika nchi inayojigamba kuwa na utawala wa kidemokrasia, halafu zikaweopo dalili za vyombo vya dola na mahakama kutumika vibaya na hasa kuridhia kile kinachoonekana kama utashi wa kisiasa.
Mpaka sasa viongozi wa Uamsho hawana kosa mpaka pale itapothibitishwa bila ya wasi wasi wowote na mahakamani kuwa shutuma zinazowakabili ni za kweli na sio za kusingiziwa au kubunia.
Watu waliokabiliwa na mashitaka ya kuingiza dawa za kulevya ambazo zinaathiri maisha ya mamia ya watu, waliodaiwa kuiba mabilioni ya fedha, waliodaiwa kufanya uzemba wa meli kuzama na watu wengi kufa na wanaosemekana wameajiri wafanyakazi hewa na kuitia hasara serikali wamepata dhamana.
Ni muhimu kuelewa kwamba dunia ina tuangalia na kutucheka. Tufanye mambo mezani na kutumia hekima na busara.
Vile vile tuelewe kwamba dunia inatuangalia na hapo tutakapolaumiwa kwamba tuliziendesha mahakama zetu hovyo tusije tukasema tunaonewa.
Tujuwe kuwa hatimaye tutapanda tunachovuna, lakini historia itatukumbuka baadhi yetu kuwa tulikataa kupalilia mbegu mbaya.
Tanzania Daima

It`s time for CCM radicals to mature

BY FATMA A. KARUME
As we were catching up with some local gossip on the telephone, the only sensible way to communicategiven Dar es Salaam’s horrendous traffic congestion, a female friend of mine informed me of her absolute sadness over the death of her friend’s father.
Taken aback by her reaction, I stated, “I did not think that you were that close to the deceased”. Her calm and wistful response was “Not really, but you know the last time I met him, he said such wonderful things about my father.” It goes without saying that my friend adores her father and knowing her father I can attest that the feeling is mutual. She is no different from all the girls who have loving and doting fathers. We love to hear good things about our fathers.
Until his retirement, my friend’s father was a businessman and I very much doubt that she has ever experienced picking up a paper and reading an article penned by someone like me with a negative opinion about her father, which he wishes to air publicly; or listening to the speech of a member of the opposition aimed at annihilating any political credibility that her father may have; or worse still listening to the speech of a member of her father’s party throwing verbal missiles at her father in order to gain political mileage.
But, as the daughter of a prominent politician in Tanzania,I have experienced all of this and more. I am not writing because I want any body’s sympathy, for I understand fully that public criticism is part and parcel of a politician’s life, and actually I think it should be encouraged, hence the reason I took up the pen. What I take umbrage to are lies but even these I have lived through. There is an essential prerequisite to being the daughter of a politician and that is a thick skin. Without a thick skin, I am afraid to say, politician’s daughters would all be quivering psychological messes. Over the years, mine has metamorphosed and become as thick as the hide of an old elephant.
A week or so ago, CCM concluded its 8thCongress with much fanfare. Khadija Kopa, a taarab guru, serenaded the 2400 or so delegates, their wives and supporters all dressed in the green and yellow CCM colours and packed in a conference hall in Dodoma. There was a lot of CCM flag waving, dancing and general merry making interspersed with the serious business of choosing the new CCM office bearers from the Chairman of the party to 20 members of the National Executive Committee. The 8thCCM Congress also marked the end of AmaniAbeidKarume’s 10 years tenure as the Vice Chairman of CCM for Zanzibar. For those who are not aware, other than being the past president of Zanzibar, I like to think tongue in cheek that AmaniAbeidKarume is more famous for being my father.
On the evening of 14 November 2012, I switched on the television with the specific intent of watching AmaniAbeid Karume bid CCM his farewell as the outgoing Vice Chairman for Zanzibar. If truthis to be known I wanted to hear him thank my mother who has stood by him solidly for 44 years.
So I listened to Abraham Kinana’s pronouncement of the CCM resolutions; watched the delegates including my mother dancing to Khadija Kopa; listened to Pius Msekwa’s goodbye speech and finally Amani Karume stepped onto the podium and commenced his speech.
Karume’s farewell speech has been the most discussed and analysed speech of the 8th CCM Congress. So it is not my intention here to analyse or discuss the speech, as I am in the privileged position of knowing exactly what he meant, neither is it my intention here to defend his speech, for there have been hundreds of lines written and thousands of words spoken in support of his speech.
I seek here to analyse what I consider to be the root of the negative reaction that his speech caused in some members of CCM Zanzibar.
As I sat listening to his speech and knowing him as well as I do, I knew he was unable to conceal the happiness he felt at what he considers to be the successful conclusion of more than 10 years of service to CCM, but it was also his moment of public reflection and presentation of his parting wish list. There was nothing controversial in what he stated, for he discussed the history of CCM, the Government of National Unity in Zanzibar, the Constitutional Review Process; the responsibility of governance and good governance; and his pleasure at seeing young faces emerging in the CCM hierarchy.
In a nutshell, on the history of CCM, Karume reminded the nation that CCM is an amalgamation of two parties—the Afro Shirazi Party from Zanzibar and TANU from Tanganyika that decided to merge and consequently the ideals of its predecessors should not be forgotten, in particular ASP’s foundation policy aimed at observing the Universal Declaration of Human Rights; eradicating all forms of racial discrimination etc…
In relation to the Government of National Unity, Karume observed that this was a choice that was made by the people of Zanzibar by a 64% majority vote in a referendum, which led to an amendment of the Constitution of Zanzibar and therefore CCM must respect this choice.
With regard to the on-going Constitutional Review Process, he asked members of his party to allow people to express their views freely in particular on the question of the nature of the Union between Zanzibar and Tanganyika, and this freedom can only be exercised where authorities showed restraint.And finally, he counselled CCM that it needs to win the hearts and minds of the people, if it is to remain relevant, and this requires governance by law and humility and not through intimidation.
Frankly, I am not going to apologise for stating publicly thatAmani Karume is a man after my own heart especially given the fact that after all this he remembered to thank my mother. Having alerted you about my relationship with Amani Karume and the particular soft spot that he holds in my heart, I have discharged my duty and as we say, “caveat emptor”.
However, I was astounded with the venom with, which some members of his own party reacted to his speech. For those who follow the news will know that some CCM members were so angered by this speech that they decided to tear downKarume’s poster in Michenzani, Zanzibar.
Why should some groups within CCM in Zanzibar be so incensed by words which did nothing more than explain that the party’s mandate to govern comes from the people, and it is these people who must be respected as well as be allowed to express their views openly? I fear that this is an unfortunate consequence of the misunderstood history of CCM and our country.
On the part of Zanzibar, CCM’s predecessor the Afro-Shirazi Party came into power after a revolution and until the Constitutional Amendment of 1992, CCM’s mandate to govern Tanzania was protected by the Constitution. CCM may not have had a Godly given right to govern, but in a non-secular state, such as the United Republic of Tanzania, a Constitutional right was as close to a God given right as CCM could get. Before the amendment, article 3(1) of the Constitution of the United Republic of Tanzania used to read as follows:
“The United Republic is a democratic and socialist state which has one political party”.
No prizes for guessing, which party the “one political party” referred to in the Constitution was.
My view is that amongst some members of CCM Zanzibar, there is an unfortunate disconnect between reality and their personal beliefs and wishes.
This disconnect is emphasised by the now common site in CCM Zanzibar meetings of a group of about 50 or so ladies dressed in CCM colours who are always strategically seated by the organisers in the very front of the audience and who are then prompted like marionettes by someone to start chanting “Commando!!! Commando!!! Commando!!”.
This chant may deceive the uninitiated into believing that these ladies are die-hard supporters of Salmin Amour the CCM President of Zanzibar 1990-2000 who referred to himself as “Commando”, had no patience for the opposition,CUF, and made his impatience categorically clear by imprisoning without trial, some 20 high profile CUF members.
Of course those in the know understand the message, which the puppet masters are sending very clearly indeed. The puppet masters want a CCM Zanzibar with a “Commando” at the helm, who will handle all ‘enemies’ with the iron fist they so deserve. There are those lurking in the dark recesses of the radical wings of the party who still believe that they have an absolute right to govern because they saved Zanzibar from the Sultan and the constitutional amendments seem to have left them bewildered and rather lost in this world of competitive politics where Tanzanians get to choose which party should govern them. Well at the risk of bursting theirodd bubble those who saved Zanzibar from the clutches of the Sultan are either dead or too old and they certainly did not lead a revolution so that some opportunistic upstarts could forever entrench themselves on the Sultan’s empty thrown.
After every five years we require all political parties to put their best candidates forward and parade them before us in a bizarre beauty contest which is the hallmark of democracies the world over, and we get to pick to which beauty we hand the crown.
Lest the winner makes himself too comfortable at Ikulu either in Zanzibar or Dar es Salaam, we require him to parade himself before us five years later, when we can overlook him and proceed to pick someone else to wear the coveted crown and take the prize money.
If he is fortunate to win and wear the crown twice, as a matter of principle we must discard him at the conclusion of his 2nd term in office with a nice pension in hand of course and we move on to the next beauty. Could it be that the radicals in CCM are very aware of their inadequacies and fear that in a political beauty context, no voter will find them attractive?
To make matters more complicated, in the case of Zanzibar, the winner of the crown and the first runner up are obliged to share the prize money. Zanzibaris now expect the winner to cooperate and work hand-in-hand with his competitor. This of course requires the two previous opponents to show each other mutual respect both during the campaign trail and after the elections and to put the interests of Zanzibar first.
A fitting punishment I say, meted out in a referendum approving a Government of National Unity by 64 percent of the voting population who were clearly far too tired of the divisive politics used and abused by both CCM and CUF in Zanzibar and the tiresome and predictable cries of foul play every time we came out of an election.
Unfortunately, there are some Zanzibar CCM members who are suffering from amnesia and have conveniently forgotten the various constitutional amendments leading to the GNU; there are others who are so unused to being restrained in this manner and are restlessly champing at the bit, impatient to see the end of whatever this mass of confusion they blame AmaniAbeidKarume for allowing to take root; and there are those who have accepted the wishes of Zanzibaris and to the radicals the latter are traitors of whatever abhorrent cause they adhere to.
In a recent CCM meeting in Zanzibar, CCM radicals used abusive and racially inflammatory language reminiscent of the language used pre-revolution against none other than moderate CCM members, oblivious of the fact that the revolution was the result of race inequalities and eagerly opening past wounds in an uncouth and clumsy attempt at gaining political mileage.
As a Zanzibari of both African and Arab descent, whose Arab great grandfather was murdered in prison immediately after the revolution for nothing more than his political beliefs and whose African grandfather was assassinated 8 years after the revolution again for nothing more than his political beliefs, I am not impressed. This is a game of high stakes, which can only result in blood loss.
It is time for the radicals within CCM Zanzibar to grow up, and realise that this is not a school playground where the bully gets everyone’s lunch money.
Forty-eight years after the revolution, Zanzibar has changed irreversibly. The majority of Zanzibaris are under 40 years old. They did not live the revolution nor the divisive racial politics that led to the revolution in Zanzibar. Our politics cannot and should not remain in the past but our history should be used to inform us of where we were so that we may know where we need to go and we may learn to avoid malignant politics.
As CCM Zanzibar is being pulled by a radical wing that is becoming more prominent, so CUF is taking up the centre ground in the politics of Zanzibar. If CCM Zanzibar wants to reclaim the beauty crown in 2015, it must reform itself and fight for the centre ground because it is the votes of moderateZanzibaris that will make the next president of Zanzibar.
Ms. Karume was called to the Bar in the Middle Temple and is an advocate of the High Courts of Tanzania and Zanzibar. She is presently Litigation Partner with IMMMA Advocates in Dar es Salaam.

Wednesday 21 November 2012

Wahafidhina CCM wanapoikana misingi ya TANU, ASP

KATIKA kitabu 'Tujisahihishe' kilichoandikwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1962 ukurasa wa pili, anaeleza dhana nzima kuhusu ukweli.
Anasema, “Ukweli una tabia moja nzuri sana. Haujali mkubwa wala mdogo, haujali adui au rafiki wote kwake ni sawa. Pia ukweli una tabia ya kujilipiza kisasi kama ukipuuzwa.
“Ukiona nataka kulipiga teke jiwe kwa kuwa nafikiri kuwa ni dongo au mpira, natumaini utanionya.
“Lakini nikilipuuza onyo lako kwa sababu eti wewe ni mdogo au kwa sababu sikupendi, nikalipiga teke, basi litanivunja dole, japo ningekuwa nani.
“Ukweli haupendi kupuuzwa puuzwa! Wakati mwingine mtu tunayempinga huwa ana makosa kweli, lakini hoja tunazozitoa ni za kinafsi na hazihusiani kabisa na hoja zake.
“Nikisema mbili na tatu ni sita nakosa. Lakini ni bora kunionyesha kwamba pengine nafikiri tunazidisha kumbe tunajumlisha.
“Ni kweli mbili mara tatu ni sita, lakini mbili na tatu ni tano, siyo sita.
“Lakini ukijaribu kuwashawishi wenzetu wakatae mawazo yangu na kukubali yako kwa kusema meno yangu ni machafu, au natoa kamasi daima, utakuwa unatumia hoja ambazo hazina maana.
“Huu ni mfano wa upuuzi, lakini mara nyingi hoja tunazotumia kuwashawishi watu wakatae mawazo ya wale tusiowapenda, au kukubali mawazo yetu, huwa hazihusiana kabisa na mambo tunayojadili,” anasema Mwalimu katika kitabu chake hicho.
Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume katika Mkutano Mkuu wa nane wa CCM Mjini Dodoma uliomalizika hivi karibuni analia na mtindo wa baadhi ya watu ndani ya chama kupuuzwa hata kama wanasema ukweli.
Anasema kumezuka mtindo ambao sio uliojenga misingi ya TANU na ASP wa baadhi ya watu kupuuzwa wakati wa kutoa maoni au kuchangia hoja mbalimbali, na wakati mwingine kupachikwa majina ya ajabu ambayo hayahusiani kabisa na hoja inayojadiliwa.
Karume anahimiza kuvumiliana katika utoaji wa maoni kuhusu Katiba kwani watu wamegawanyika kuhusiana na kile ambacho wanataka kiwemo katika Katiba mpya hususani suala la Muungano.

Anasema kuna watu ambao wanapendekeza Muungano uliopo udumu na wapo ambao wanataka uwe wa Serikali mbili pia kuna ambao wanapendekeza ziwe mbili lakini za mkataba.
"Wote hao ni haki yao muwastamilie, muwavumilie na wengine bungeni nimesikia wanataka Serikali tatu, si hiyari yao?" anasema Karume katika mkutano huo huku miguno na sauti za kuzomea zikianikiza katika ukumbi wa mkutano huo.
Rais huyo mstaafu wa Zanzibar hafichi hisia zake na badala yake anaeleza kuhusiana na vitendo vya wanaCCM kukosa uvumilivu wa kisiasa "uvumilivu unakushindeni hapa...! na hapa tupo wapi? Katika Mkutano Mkuu wa CCM, si mnaona?" anasema.
Anawataka wanaCCM hao wajifunze uvumilivu akiamini kuwa wanaweza, tena wanaweza vizuri sana na anawahoji iwapo maoni hayo wanakusanya wao CCM, na vipi wasiwaache waliopewa jukumu kutekeleza wajibu wao na wao kusubiri matokeo.
"Watu waachwe watu wafanya kazi yao kisha tutajua, lakini jambo la kushangaza wakitokea watu wakatoa maoni tofauti hao wanaitwa majina ya ajabu," anasema.
Anauliza vipi iwe nongwa na mtu aitwe majina ya ajabu jambo ambalo anasema sio haki wala utu na mambo kama hayo hayapo katika msingi ya TANU na ASP, vyama ambavyo vimezaa CCM.
Karume anadai kuwa Zanzibar kuna watu ambao wanawatisha wenzao kuwa mawazo yao yana lengo la kurejesha utawala wa kisultan Zanzibar.
Anasema kuwa chama hicho hivi sasa kina vijana wadogo wengi ambao hawajui kitu kuhusiana na masuala mbalimbali ya kisiasa na wanatakiwa kujifunza kwa watangulizi wao, jambo ambalo wengi hawalifanyi.
"Vijana wapya mlioingia jifunzeni kutokana na viongozi wenu waliowatangulia ili muimarishe chama chenu na matumaini ya chama chenu yapo mikononi mwenu," anasema.
Karume anasema ukweli kuwa kuna maelfu ya wanaCCM ambao ni majeruhi wa kisiasa ambao kutokana na maoni au michango yao wakati wa kujadili hoja mbalimbali likiwemo suala la Katiba.
Mifano ipo ya wahanga wa mfumo huo mbovu ndani ya chama lakini la msingi ni kuwa huyo anayesakamwa kutokana na kutoa maoni yake katika Katiba anafanyiwa hivyo kwa faida ya nani na ili iweje?
Karume ana hoja na hata wanaopingana na maoni yake wanajua hilo na hali hiyo kwa kiasi kikubwa inachagizwa na ukweli kuwa kuna wajasiriamali ambao wameijingiza katika siasa, wakiwamo vijana na hata watu wazima ambao hawajui dhana nzima ya siasa.

Pia watu hao ndio ambao hawajui chimbuko la chama wanachodai kuwa wao ni wanachama, kilipo na wapi wanaweza wakakipeleka kwani misingi ya TANU na ASP.
Misingi ya vyama hivyo inatajwa kuwa ni pamoja na pamoja na kupigania na kudumisha uhuru na raia wake.
Kulinda heshima ya kila binadamu kwa kufuata ipasavyo kanuni za tangazo la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu la Mwaka 1948 na kupinga ubaguzi wa namna yoyote na kuiwezesha nchi kuondoa ujinga, umaskini na magonjwa kwa njia ya kushirikiana.
Karume anaposema vijana wa sasa hawajui lolote anajua anachokisema kwani wanachama wanapovunja kanuni na Katiba ya chama chao kwa sababu yoyote ile ni wazi kuwa wanaofanya hivyo kwa maslahi binafsi na wala si ya umma.
Chuo cha Siasa Kivukoni au taasisi nyingine ya namna ile iwapo ingekuwepo na kutumika kama ilivyokusudiwa awali ni wazi kuwa hali ya wengine kunyooshewa vidole kutokana na kutoa maoni yao katika hoja mbalimbali ikiwemo ya Katiba isingekuwepo.
Pamoja na yote, wanaCCM na hata wanasiasa wengine lazima wakubali kuwa kila mmoja ana haki ya kuwa na maoni yake katika masuala mbalimbali, hivyo sio busara kuminywa uhuru na haki za watu ambazo zimeainishwa katika Katiba na matamko ya umoja wa mataifa.
Chanzo: Mwananchi

Thursday 15 November 2012

Wapeni uongozi wapenzi wa busara

Hekima za Barazani kwa Ahmed Rajab
HUU ni wakati wa Wazanzibari kusimama na kuwashika masikio viongozi wao. Chokochoko zinazofanywa chini kwa chini na matamshi ya uchochezi tuliyoyasikia hivi majuzi yakitamkwa hadharani, tena kinaganaga, na viongozi wachache wa CCM/Zanzibar ni mambo ambayo hayawezi kuvumiliwa katika karne ya 21.
Hotuba zilizojaa chuki za kikabila na vitisho vya kutumia nguvu na zenye lengo la kuichafua hali ya utulivu iliyopo nchini tangu papatikane Maridhiano ni mfano wa matamshi ya uchochezi (‘hate speech’).
Kanda za video za hotuba hizo ni ushahidi madhubuti wa kuweza kuwafungulia kesi wenye kuyatoa matamshi hayo. Inasikitisha kuona kwamba viongozi wakuu wa chama cha CCM wamekaa kimya wakiwasikia viongozi wa ngazi za chini wakitoa matamshi ya usaliti na uchochezi. Inasikitisha zaidi kuiona Serikali ya Umoja wa Kitaifa na hasa vyombo vyake vya kisheria pia imekaa kimya bila ya kuwachukulia hatua wanaohusika au hata angalau kuwakemea.
Nina hakika kwamba lau matamshi kama hayo yangekuwa yametamkwa nchini Kenya basi wanasiasa hao wangelikwishajikuta mahakamani wakijibu mashtaka ya uchochezi.
Ingekuwa hivyo kwa sababu Kenya ya leo ina katiba ambayo, ingawa ina madosari yake, haivumilii mambo ya kipuuzi lakini yenye hatari kama hayo. Kadhalika Kenya ina asasi za kiraia pamoja na vyombo vya habari vilivyo macho vinavyokemea dalili zozote zinazoweza kusababisha mauaji ya raia.
Vivyo hivyo, vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, vitendo vinavyofanywa na vyombo vya dola kuwadhalilisha wananchi navyo pia haviwezi kuvumiliwa katika jamii inayojinasibisha na mfumo wa demokrasia.
Katika mfumo wa demokrasia tunaosema kuwa tunauiga dola lazima iwe na uhalali. Na uhalali huo unaweza kujengwa juu ya mihimili mitatu: utawala bora, uongozi stadi na ufanisi katika kuwakidhia wananchi mahitajio yao.
Katika hali hii iliyopo sasa utawala bora maana yake ni kuvifanya vyombo vya kisheria vya dola vichukue hatua zinazostahiki bila ya upendeleo. Uongozi stadi maana yake ni kuwa na viongozi wanaojitokeza wazi na kuchukua hatua au kukemea pale mambo yanapoonekana kuwa na dalili ya kwenda kombo bila ya kujali iwapo wenye kusababisha hayo ni watu wa chama chao au la. Na kuwakidhia wananchi mahitajio yao ni kuwapatia raia wanachokihitaji kwa ustawi wao.
Wazanzibari wamechoka kuhasimiana kisiasa. Wameona jinsi uhasama wa kisiasa ulivyowahasirisha kwa kipindi cha miongo kadhaa. Ndiyo maana zaidi ya thuluthi mbili yao walioshiriki katika kura ya maoni ya kihistoria wakakubali pawepo Maridhiano na paundwe Serikali ya Umoja wa Kitaifa baina ya vyama vikuu viwili vya kisiasa Visiwani humo yaani CCM na CUF.
Wazanzibari wengi walikuwa na matumaini mema ilipoundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Novemba 2010. Walihisi kwamba kupatikana Maridhiano na kuundwa kwa serikali ya aina hiyo kutaipatia Zanzibar amani, utulivu wa kisiasa, maendeleo na umoja wao. Kwa sababu hizo waliiunga mkono moja kwa moja serikali mpya ilipoundwa.
Zanzibar ilipiga hatua kubwa ya kuelekea mbele yalipopatikana Maridhiano na ilipoundwa serikali hiyo. Sasa kuna wasiwasi kwamba inaweza ikarudi nyuma. Hivyo ni jambo la busara kwamba viongozi wa Kizanzibari na waliomo kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa wakabiliane vilivyo na changamoto iliyopo na waendelee kuyatafutia ufumbuzi matatizo yote ambayo lazima yataendelea kuzuka.
Msimamo wao uwe ni wa kuangalia mbele, na si nyuma. Tena uwe ni msimamo wa kujitolea kuziondosha tofauti zote zilizo ndani ya jamii kwa njia ya kindugu ili waweze kuyatetea maslahi ya Zanzibar na ya watu wake wote.
Haya yote ni muhimu hasa kwa vile mustakbali wa Zanzibar huenda ukaamuliwa katika kipindi cha kasoro miaka miwili ijayo kufikia 2014 pale utapomalizika huu mchakato wa sasa wa kulipatia taifa katiba mpya.
Kwa hivyo, ni muhimu kwamba mawaziri wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa wawe wanayatetea na kuyapigania matakwa ya raia waliowachagua na wasiende kinyume nao kwani endapo zoezi hili la katiba halitokuwa na matokeo ya kuwaridhisha wengi wa Wazanzibari basi kutaendelea kuwako na manung’uniko ya kisiasa. Tena zoezi hilo litakuwa limeshindwa kuutafutia ufumbuzi ule mgogoro wa muda mrefu kati ya Zanzibar na Serikali ya Muungano.
Kwa hili ni muhimu kwamba Wazanzibari wawasihi viongozi wao wa vyama vyote vya kisiasa wafanye mambo kwa busara na wavumiliane kisiasa. Kama kuna tofauti zozote zinazozuka ndani ya Serikali basi watumie njia za mazungumzo na za kidemokrasia ili wapatane na kuhakikisha kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa inafanikiwa katika utekelazaji wa sera zake, hasa zile zinazohusika na maslahi ya Zanzibar na ustawi wa Wazanzibari wote bila ya kujali mielekeo yao ya kisiasa.
Inafaa Wazanzibari wawakumbushe viongozi wao wasia wa Plato, yule mwanafalsafa wa Kiyunani, aliyewahi kusema kwamba: “Wanadamu kamwe hawatoona mwisho wa matata mpaka pale wapenzi wa busara wataposhika madaraka ya kisiasa, au pale wenye madaraka watapokuwa wapenzi wa busara.”
Wawakilishi wa Kizanzibari ndani ya vyombo vyote vya maamuzi kuhusu suala la katiba wanabeba jukumu kubwa. Hawa ni wale wenye kuiwakilisha Zanzibar ndani ya Serikali ya Muungano, ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa na hata wale wawakilishi 15 wa Kizanzibari walio katika Tume ya Katiba.
Ikiwa watafanya kazi zao bila ya kuuzingatia uzalendo wao na kwa maslahi ya Zanzibar na badala yake wakijiachia waongozwe na mazingatio ya maslahi yao binafsi au ya vyama vyao basi wataiangusha Zanzibar na Wazanzibari wenzao na watasababisha madhara makubwa yatayohitaji vizazi kadhaa kuyaondosha.
Chanzo: Raia Mwema

Wednesday 14 November 2012

Kamati ya Maridhiano Six

Leo nami nimeamua kutoa mawazo yangu kupitia kwenye ukumbi huu. Kwa wale wasionifahamu mimi ni Mansoor Yussuf Himid nimezaliwa Novemba 3 mwaka 1967 Kisiwa cha Unguja ni Mzanzibari kwa mama na baba , kama walivyo Wazanzibari wengine wazee wangu wana asili ya pande mbili Bara na Arabuni...
. Baba yangu mzazi ana asili ya Bara ambapo upande wa baba ni mnyasa na upande wa mama ni mmanyema na mama ana asili ya Arabuni (Oman), lakini ni mseto wa aina yake maana anadamu ya Ki-manyema,ki-somali,ki-ngazija, hali hii si ya ajabu kwa Wazanzibari bali ni kawaida tu na ndio hali inayo tutambulisha Wazanzibari.
Mimi ni Mtanzania kama walivyo wazee na ndugu zangu na wanangu na mke wangu Asha Abeid Amani Karume, kama unajiuliza Karume yupi ni huyo huyo unayemfikiria wewe ni Marehemu Abeid Amani Karume, Baba wa Taifa la Zanzibar , mungu amlaze pema peponi na amsamehe kwa mapungufu yake na amjaalie aendelea kutajwa kwa kheri na wema kama anavyo tajwa sasa.
Marehemu mzee Karume ana haki ya kuitwa Baba wa Taifa la Tanzania pia na wala mshishangae kwani Marekani Taifa la kupigiwa mfano kwa historia na misingi yake imara ya haki za binadamu,demokrasia na utawala bora , wana baba wa Taifa (Founding fathers) zaidi ya mmoja.
Kwa wengine nikiwemo mie kutothaminiwa kwa marehemu Bwana Abeid Amani Karume kwa kuitwa muasisi tu tena wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wala sio Nchi au Taifa la Zanzibar au Tanzania ni kutothamini mchango wake katika kuasisi Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani bila ya Zanzibar hakuna Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ni sehemu ya kero za Muungano wetu.
Tuelewe kuwa kwa kumthamini marehemu Sheikh Abeid Amani Karume, hatuondoshi nafasi ya Marehemu Mwalimu Julius kambarage Nyerere hata kidogo,nafasi ya Mwalimu ni kubwa mno (iconic) kwa wengine iliotukuka (saintly) sio tu kwa Tanzania na Afrika bali mwenyezi mungu amemjaalia Mwalimu kuthaminiwa na kupendwa na mataifa duniani kote,mpaka hii leo miaka kadha baada kufariki kwake, sababu za kupendwa kwa Mwalimu akiwa miongoni mwa viongozi wachache duniani wenye hadhi kama yake ni nyingi kwa leo si dhamira yangu kueleza wasifu wa Marehemu Mwalimu Nyerere.
Sasa nieleze nilioyakusudia. Historia ya Zanzibar imeandikwa sana sina haja kuirejea, dhamira yangu ni kuzungumzia hali ya kisiasa, kijamii Zanzibar ya sasa na mchakato wa marekedisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Hivi sasa Zanzibar ina Serikali yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa kwa jina fupi SUK au la kizungu 'Government of National Unity' (GNU) Serikali hii haikuja tu kwa sababu kulikua na watu wana mapenzi nayo au kwa kutaka kukisaliti Chama Cha Mapinduzi na Mapinduzi yetu Matukufu ,hapana palikua na haja tena haja hiyo ilikua kubwa na ya msingi.

Haja hiyo imetokana na Historia ya Zanzibar na siasa za vyama vyetu na Mapinduzi yenyewe, haja ya kujenga misingi ya siasa na utawala Zanzibar inayo heshimu haki za binadamu,utawala ulio bora,Wazanzibari kuhakikishiwa uhai wao ,Uhuru wao, fursa na haki ya kujiendeleza ndani ya Nchi yao na kupata hudumu za kijamii na kushiriki siasa bila ya kubaguliwa, ambapo la muhimu kuliko yote ni Wazanzibari wote bila ya kujali kabila,dini,rangi,eneo analotoka kuwa sawa mbele ya sheria na utoaji wa haki, misingi hii pamoja na kuitangaza Zanzibar kuwa Jamhuri ili kuondosha nafasi ya Wazanzibari kutawaliwa, misingi inayoheshimu haki za binadamu na isiyokuwa na chembe chembe za kibaguzi na utengano ndio iliokuwa ya mwanzo kutangaziwa Wazanzibari na Marehemu mzee Abeid Amani Karume baada ya Januari 12 mwaka 1964.

Zanzibar kwa miaka mingi kabla na baada ya Mapinduzi iligubikwa na inaendelea kugubikwa na siasa za chuki,hasama na ubaguzi na zisizo toa nafasi kwa binadamu kustahamiliana , dhamira ya Mapinduzi ni kuondosha mazingira hayo na kuwaunganisha Wazanzibari, kwa bahati mbaya hali hii ya utengano iilijirudia upya baada ya ujio wa vyama vingi mwaka 1992, miafaka mingi tumepitia bila ya mafanikio na nchi hii kushindwa kutafuta dawa ya kudumu.

Yote hayo (haja) ni katika kutafuta dawa ya kudumu ili Wazanzibari waishi kwa salama,kwa upendo, kuheshimiana, kustahamiliana na muhimu zaidi kuvumiliana,na siasa zao zisiwe ndio chanzo cha kugawanywa kwao bali siasa iwe chachu ya maendeleo yao na waweze kuishi kwa kushiriki siasa na kupenda vyama vyao bila ya kuchukiana,kubaguana na kuuwana ,na vyama hivyo visiwe sababu ya kuhasimiana kwao bali sera,ilani na itkadi za vyama ziwe dira ya maendeleo yao.

Kwa msingi ule ule wa demokrasia Wazanzibari waendelee kuendesha siasa kwa kukubali kutokukubaliana kiungwana na kwa kuelewa kwamba nguzo yao ni Zanzibar na wote ni Wazanzibari tofauti ni vyama vyao tu, lakini kila mmoja ana haki sawa na mwenziwe kuchagua apendako bila ya kubatizwa majina mabaya au kutengwa na sehemu ya jamii au kubughudhiwa na mtu yoyote iwe Chama cha siasa au Serikali na wakielewa kwamba vyama vyote vya siasa mwishowe vinahitaji watu na watu wanahitaji maendeleo ,kujitambua,usalama,amani na muelekeo thabiti wa Nchi yao.

Malumbano yasio na msingi isipokua huyo Mpemba na huyo Muunguja, huyu CCM na huyu CUF hayana tija wala mwisho mwema,Vijana wa Kizanzibari hawapati kazi ,elimu,huduma muhimu za kijamii wala matumaini ya maisha yao kwa U-Pemba na U-Unguja na kupelekwa pabaya na wanasiasa wanao hubiri chuki, ubaguzi na utengano,kwa bahati mbaya wengi wetu wanasiasa tumetenda na tunaendelea kutenda dhambi hizo tena wa vyama vyote CCM na CUF.

Dhana iliyopo ni kwamba wahafidhina wapo CCM tu,si kweli hata CUF wapo,zao la uhasama,ubaguzi na chuki ni watu kuvunjika moyo (frustrated) kukosa muelekeo na imani juu ya nchi yao na viongozi wao na nchi yetu kuendelea kuwemo ndani ya mzunguko (vicious circle) usio na mwisho wa hasama,chuki,ubaguzi, na kukosa muelekeo,na kuaminiana, wapi tunakotoka, wapi twendako,yepi ya maana tunataka kuyatekeleza na nini hasa dira ya Nchi yetu na nini tunataka kurithisha kizazi kijacho,kauli mbiu za wanasiasa zinazo ashiria ubaya na mivutano isiokwisha au Zanzibar yenye muelekeo na matumaini kwa walio hai leo na kizazi kipya?

Wajibu wa watu katika jamii ni kuwiana hisani,usawa,adabu,heshima na mapenzi na kwa kiungo hichi cha johari ya kuwiana Wazanzibari tuliweza kuridhiana na kuungana katika ujenzi wa nchi yetu. Kama nilivyosema awali,wajibu huu hapa Zanzibar ulimezwa na siasa za chuki, ubaguzi wa kutisha ambapo watu pengine wa kiambo kimoja au hata familia moja waliwiana chuki,kisasi na makamio huku pumzi ya kila mmoja ilijaa hofu,kushupaliana, sumu juu ya sumu.Inshaallah Mwenyezi Mungu atuepushe na ubaya na hatari hiyo leo na twendako.

Hatua iliyo fikiwa sasa ya kujenga Zanzibar mpya baada ya ujasiri na muono thabiti (vision)wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kutafuta dawa ya kudumu itakayo ondosha kabisa siasa za chuki,hasama na za kibaguzi ziliopo Zanzibar ilikuwa ni hatua sahihi yenye uzalendo ndani yake kwa ujenzi wa Zanzibar mpya na tuitakayo.

Dk. Jakaya Kikwete tulimlaani sana wenziwe huku Zanzibar na yeye kumwita msaliti wa Mapinduzi kwa kutaamka kwamba Zanzibar kuna mpasuko wa kisiasa na hali hiyo inamsononesha na kubwa zaidi kwamba hali hiyo inahitaji dawa, tena dawa chungu mno ya kushirikiana na adui mpinga Mapinduzi? lakini ukweli ukaendelea kubaki kuwa ukweli na wahenga wamesema ukweli ukidhihiri uongo hujitenga,muda ukapita busara zikatawala na tulio wengi tukakubali ukweli kwamba chuki,ubaguzi,hasama,vifo na majonzi ya mwaka nenda mwaka rudi sio njia sahihi,bali tunawajibu wa kutenda yale pengine tunayoyachukia, lakini kwa dhamana tulionayo na ubinadamu tunawajibu wa kubadilika.

Kwa upande mwengine,Ujasiri na upeo mkubwa wa Dk. Amani Abeid Karume Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (mst) ni kutambua na kukubali kwamba Nchi anayoiongoza inaumwa na siasa zake zinakwenda kinyume na dhamira ya kweli ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964 na yeye kutokukubali kumuachia mrithi wake maradhi aliorithi yeye huku akijua kwamba hatua hiyo itamchukiza sana sana kwa baadhi ya wenziwe walio wahafidhina (zealots) pamoja na mazingira hayo magumu yeye alichukua hatua ngumu lakini sahihi ya kuwataka Wazanzibari wenyewe wafanye maamuzi juu ya hatma ya Nchi yao,na kupitia kura ya maoni Wazanzibar walio wengi wakamua kwa sauti moja kwamba wamechoka na siasa za mivutano na hasama,kiongozi makini na mwema anapaswa kuongoza sio kuongozwa na huo ndo mtihani wa uongozi,tuseme tusemavyo lakini Dk Karume na Maalim Seif wamefuzu mtihani huo wa uongozi.

Huku kwetu Zanzibar ni dhambi kubwa kumtaja tu kwa vizuri kiongozi wa upinzani ,seuze kummiminia sifa, hiyo ni dhambi kubwa zaidi isio na mfano,humalizii tu kuitwa msaliti wa Chama chako na Mapinduzi bali utaitwa Hizibu(Zanzibar Nationalist Party-ZNP) namba mbili, namba moja akiwa Jamshid mwenyewe (Sultani wa mwisho Zanzibar) , Hizbu likiwa ndo tusi baya na la mwisho kupewa mwanasiasa Zanzibar hasa anaetokana na CCM ,lakini ukweli ni kwamba Maalim Seif Sharrif Hamad anastahili kila sifa ya kuacha utashi wa nafsi yake na wa Chama chake kwa kuweka maslahi ya Zanzibar mbele, na kukubali dhamira njema ya CCM na hatimaye kushirikiana na CCM kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kujenga mustakbal mwema wa Zanzibar na kizazi chake.

Siku zikapita,miezi ikayoyoma na hatimaye ni Rais Kikwete yule yule kwa kuthibitisha umakini,busara na wingi wa hekima ya uongozi wake amethubutu,ameweza kuunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nilimsikiliza kwa makini wakati akizindua Tume ile pale Ikulu Dar es Salaam kubwa alilotuasa ni kuweka mbele uzalendo na maslahi ya Taifa letu kwa kila mmoja kutoa maoni anayodhani yatasaidia katika kupata katiba mpya.

Kwetu sisi Wazanzibari katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatugusa katika baadhi ya mambo ambapo kati ya yote hayo kilele cha umuhimu ni suala zima la Muungano ambao umetimia miaka 48 tangu kuundwa kwake mwaka 1964. Ukelele wa mabadiliko ya muundo wa Muungano ulikuwa katika kila pembe ya viunga vya Zanzibar, kule Mtende Makunduchi, Kijini, Kibuteni,Jambiani, Ndijani, Uzini, Bambi, Umbuji, Pongwe,Uroa,Chwaka,Mkwajuni, Nungwi, Matemwe, Limbani, Jadida, Wete, Ziwani, Wambaa, Chake Chake ilimradi kila pahala.

Kwa bahati mbaya,tunataka kurudishwa kwenye siasa za chuki,hasama na kutoheshimiana na kuvumiliana hata kwa mawazo,kila anaezungumza kwa kutaka mabadiliko katika mfumo wa Muungano basi tayari ni msaliti wa Chama chake na Mapinduzi, utafikiri Chama na Mapinduzi ni hati miliki ya baadhi yetu,wengine sote sio,huna haki ukiwa Mtanzania na Mzanzibari kueleza kwa upeo fikra zako juu ya namna unavyotaka Muungano wako uwe kwani huu Muungano ni wa Watanzania wote kama hawakusema wao atasema nani,na kwanini tusiseme ni Haki yetu kusema,Watanzania hatukuwasemea Wakenya wakati wanarekebisha Katiba yao wamesema wenyewe.

Nakubaliana na raia wenzangu na Serikali yangu kwamba katika mchakato huu hatupaswi kukubali kutoa nafasi kwa wanao hubiri utengano, ubaguzi,udini, na matumizi ya lugha chafu na za kibaguzi pamoja na kutumia fujo kama njia ya kufikia malengo yao na wote wanaofanya hivyo wanapaswa kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria kwani tunako toka kubaya sana,hatupaswi Wazanzibari wenye akili timamu kushabikia vurugu tutajimaliza wenyewe maana wazee wanasema vita vya panzi neema kwa kunguru!

Lakini papo hapo sikubaliani hata kidogo na dhamira ya wachache kutaka kuwanyima wananchi wa Zanzibar haki na uhuru wao wa kutoa maoni yao kwa kisingizio chochote kile iwe vitisho,iwe kushurutishwa na kupangiwa,iwe kwa kubatizwa majina ya Uhizibu,usaliti wa Mapinduzi na Chama kwani naamini hatuwezi kupata Katiba na muundo wa Muungano ulio bora kwa kuviza maoni na matumaini ya watu, tukumbuke kuwa kwenye wengi hapaharibiki jambo nami naamini kwa uelewa wa wananchi hakuna jambo litakalokwenda kombo zaidi ya kuhuisha mahusiano ya kale baina ya watu wa Zanzibar na Tanganyika.

Tukifikiri vyenginevyo, tutakuwa tunazidanganya nafsi zetu na hatutafika kwani siku zote watu makini hawapaswi kuhofia mawazo ya wenziwao kwa visingizio vya wanataka kumrudisha Sultan na kuvunja Muungano! haya ni mawazo tu si risasi wala mzinga iwe Muungano wa Serikali mbili, tatu,mkataba au mfumo wowote ule mujarab utakao tuondosha hapa tulipo kwenda kuzuri zaidi penye heshima, na tunakhofia nini kwani Wazanzibari tulio wengi Muungano tunautaka na sisemi haya kwa kebehi au kujikosha na kujipendekeza hapana.

Kama husadiki pita kila pembe ya Zanzibar zungumza na Wazanzibari utapata jibu hilo hilo wapo wenye jazba na machungu yao hao watakwambia bila ya kukuficha kwamba Muungano hawautaki,lakini wengi wape na wachache usiwapuuze wasikilize, hatimae kila Mtu anataka kuheshimiwa utu wake tu! kwani kinachotakiwa na Wazanzibari ni Muungano wa haki,ulio sawa na wa heshima.

Pamoja na maelezo yote haya mimi bado nina amini kwamba Nchi yetu iko kwenye mikono salama ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein na viongozi wenziwe wakuu wa Nchi na wasaidizi wao la umuhimu kwetu Wazanzibari ni kuacha kulalamika sana na kuelewa kwamba tunapaswa kuwasaidia kwa dhati na kuwa wakweli kwa kusimama na ukweli.

Viongozi wa dini,wa jamii na sisi wa siasa tunapaswa kuacha viburi na jazba na kuhubiri na kutenda mema,hata kama yale tutakayoyasema yatachukiza kwa baadhi ,lakini yakiwa yenye manufaa kwa jamii na khatma njema ya Nchi yetu,basi ndio njia sahihi hiyo na ndio njia pekee ya kuondokana na hali tulionayo,siasa ya majibizano za kila jumamosi na jumapili zinaongeza hofu na suita fahamu tu miongoni mwa Wazanzibari ,lugha chafu,matusi,ubaguzi,hasama,udini,uchochezi haujatufikisha popote,wala hatufiki popote,ila tutaendelea kubaki na umaskini wetu na baya zaidi tutajirithisha umaskini wa roho pia.

Haya yatapita kama yalivyopita mengine kwani hufika muda katika maisha ya Nchi na watu wake siasa za kuridhiana, kuvumiliana,kuheshimiana na kujenga umoja na maelewano zikaonekana na wachache kuwa ni za udhaifu mkubwa na wanoa hubiri siasa hizo kuonekana nao ni watu wasio shupavu , lakini historia inatudhihirishia kwamba hali hiyo haidumu na haijapata kudumu popote duniani,inahitaji moyo na dhamira njema kuondokana nayo,Wazanzibari tuko wapi,vipi tanutaka Nchi yetu na Muungano wetu uwe ni suali ambalo letu sote kulitafutia jibu na tukumbuke Wazanzibari Marehemu Bwana Abeid Amani Karume kasema. Angalieni khatma!!!!

MWISHO.

Mwandishi wa makala haya ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki(CCM) Zanzibar

Tuesday 13 November 2012

Baharia Karume Aegesha Chombo Bandarini

Rais Mstaafu wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM (Zanzibar), Mhe. Amani Karume, amewapa darasa zuri la uongozi na demokrasia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa chama chake na wananchi kwa ujumla hasa kuhusiana na mwelekeo wa siasa Zanzibar. Alisema hali ya kisiasa Zanzibar ni ya kuridhisha na yenye amani na utulivu ambapo fujo na ghasia za hapa na pale zinatokana na wanaharakati na siyo wanasiasa. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ilikubaliwa kupitia vikao vya CCM lakini iliamuliwa kwa kupitishwa na Wazanzibari ambao kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ndiyo waamuzi wa mwisho wa mustakbali wa kisiasa wa Zanzibar. Viongozi wa CCM Zanzibar wasipowatendea wema wananchi watawakumbuka wakati wa uchaguzi ukifika. Ubaguzi, ubabe na kuchochea mfarakano si katika malengo ya ASP. Kila mtu aachiwe kuwa huru kutoa maoni anayoyataka kuhusiana na Mjadala wa Katiba Mpya na watu wasiitwe majina mabaya kwa sababu tu maoni wanayotoa hayaungwi mkono na baadhi ya watu. Tumewataka watu watoe maoni yao, basi tuheshimu mawazo yao. Wanaotaka Muungano uendelee ni haki yao, wanaotaka Serikali mbili kama zilivyo, wanaotaka Serikali mbili za Mkataba, wote waheshimiwe. Tume ya Katiba ndiyo iliyopewa kazi ya kukusanya maoni ya wananchi, iachiwe ifanye kazi yake. Hatimaye maoni ya walio wengi yaheshimiwe. Uongozi ni kazi nzito, na mimi nina asili ya ubaharia kupitia kwa baba yangu. Leo nakiegesha chombo salama bandarini na nina-sign off. Ni jukumu la wenzangu sasa kukipeleka chombo salama. Muhimu tujifunze kuvumiliana. Hapa kwenye Mkutano Mkuu huu, Mwenyekiti kaalika viongozi wa vyama vya upinzani na wametwambia maneno ya maana ya kutushauri. Ingekuwa Zanzibar kumefanyika yale tungeitana kila majina mabaya. Tujifunze kuvumiliana.
Chanzo: Mzalendo

Saturday 10 November 2012

Unyama huu ukomeshwe Zanzibar

Na Salim said Salim
KATIKA mwisho wa mwezi Aprili, mwaka 2005 nilieleza katika gazeti hili namna nilivyosikitishwa na kushitushwa na baadhi ya watu katika nchi mbali mbali walivyodhalilishwa, kuteswa na hata kuuliwa na vyombo vya dola kwa visingizio mbali mbali.
Vyombo vya dola ambavyo ndio dhamana vya usalama wa raia vilikataa kuhusika na kuishia kulaumu wahuni.
Lengo la makala ile lilikuwa kuieleza serikali ya aliyekuwa Rais wa Zanzibar, komandoo Salmin Amour, kwamba historia haitafumbia macho mwenendo wake wa utawala na kumtaka achukue haraka zitakazowapa nafasi watu wa Visiwani kuiona serikali kuwa ni yao na ipo kwa masilahi yao.
Hivi sasa komandoo anakumbukwa zaidi kwa vitendo vile kuliko mengine. Leo ninakusudia kurejea simulizi ile kwa vile yanayotokea Zanzibar hivi sasa yana muelekeo unaotaka kufanana na tuliyoyaona wakati wa utawala wa komandoo.
Katika makala yangu ile ya zaidi ya miaka saba iliyopita nilieleza kuwa nilipokuwa kijana mdogo ninasoma Czechoslovakia, sasa imegawika na kuwa nchi mbili za Czech na Slovak, katika mwaka 1964 nilitembelea kijiji kimoja cha Slovakia, nje kidogo ya mji wake mkuu wa Bratislava.
Nilielezwa namna ambavyo kijiji hiki kilichopo kando kando ya Mto Danube, kilivyoshuhudia halaiki ya aina yake wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia (1939-45).
Maelezo niliyoyapata kutoka kwa watu walioshuhudia halaiki ile na kupoteza ndugu, jamaa na marafiki ilinipelekea kukosa usingizi kwa karibu wiki nzima.
Maelezo yale yalikuwa juu ya namna askari wa kinazi wa Adolf Hitler, dikteta wa Kijerumani aliyesababisha vita walivyotesa watu na kutia moto nyumba huku watu wakiwamo ndani usiku na mamia kupoteza maisha.
Furaha yangu ya kutembelea Slovakia ilinitumbukia nyongo, lakini nilipata mafunzo ya namna mbavyo madikteta wanavyokuwa hawathamini maisha ya watu.
Hadithi za kusikitisha za watu wale sitazisahau daima. Sikujua kwamba ipo siku nitakaporudi nyumbani nitasikia hadithi zinazofanana kwa kiasi fulani na zile.
Nilieleza mara kadhaa nilipokuwa Addis Ababa, Ethiopia, wakati wa utawala wa Mengistu Haile- Mariam, ambaye sasa anaishi Zimbabwe kama mgeni wa rafiki yake Rais Robert Mugabe.
Niliwaona askari wa mgambo waliokuwa wakiitwa Kabele walivyokuwa wakipiga watu barabarani na majumbani. Walichokuwa wakifanya waliiga askari wa dikteta wa Haiti Papa Doc waliojulikana kama Tom Tom Makut.
Siku moja nilipokuwa Addis Ababa, katika eneo linaloitwa Markato, yaani markiti (sokoni) vijana hao waliwapiga watu wawili mpaka wakafa hapo hapo na siku ya pili yake vyombo vya habari vya serikali vilieleza kuwa vijana wale walikuwa wapinga mapinduzi na wachochezi.
Kosa lao ni kuwa vijana wale hawakuitikia na kukaa kimya pale mwanamgambo mmoja wa Kabele aliposema kwa sauti ‘Maisha marefu kwa Mengistu’.
Kila mtu alitarajiwa ajibu : ‘Aishi’. Baadaye nilikuja kupata habari kwamba mmoja alikuwa amelewa na mwingine alikuwa hasikii vizuri.
Nilikwenda Arusha ambapo nilifanya kazi kama mwandishi wa magazeti ya serikali ya Daily News na Sunday News kabla hayajataifishwa mwaka 1971.
Huu ni mji nilioufurahia sana kwani maisha yalikuwa mazuri kwa kipindi cha karibu miaka saba niliyokuwepo huko tangu mwaka 1967, mara tu baada ya kuundwa jumuiya ya kwanza ya Afrika Mashariki.
Lakini nilipotembelea Arusha mwaka 2000 kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari nilijikuta nakumbuka Czechoslovakia. Hii ilitokana na siku moja kwenda kusikiliza kesi za mauaji ya halaiki ya Rwanda ya 1994.
Sikustahamili na nilitoka nje mapema kutokana na maelezo yaliyotolewa kuonesha binadamu anavyoweza kupoteza utu wake na kuwa mnyama, katili kama nilivyowaona wanyama pindi nilipotembelea mbuga za Manyara, Ngorongoro, Serengeti na Momella nilipokuwa ninaishi Arusha.
Mashahidi walielezea mauaji na mateso yaliyofanywa na vijana wa Interahamwe yaliyoandamana na uchomaji nyumba moto huku watoto wadogo wakilia ndani walivyokuwa wakijiona wanapoteza maisha yao wakiwa hawana la kufanya.
Wakati nilipoandika makala ile kwa gazeti hili nikiwa Zanzibar nilishuhudia mambo ambayo sikutaka kuyaamini.
Siku moja baada ya kutoka Ofisi ya Tume ya Uchaguzi Kilimani, nilipigiwa simu kwenda Hospitali ya Al-Rahma iliyokuwepo masafa ya mita 300 toka mahali nilipokuwepo.
Nilipofika hapo niliona watu waliokatwa katwa mapanga kichwani, miguuni na wengine kupigwa nondo, huku wakimiminika damu. Wawili walikuwa wamepoteza fahamu. Ilinikumbusha mbali na kutoamini niliyoyaona. Picha na video za matukio yale zipo.
Jumla ya watu waliofikishwa pale wakiwa majeruhi walikuwa 10, wote taabani na nilielezwa kuwa walipigwa mapanga na nondo wakati wakingojea kujiandikisha kuwa wapiga kura katika kituo cha Kijiji cha Kinuni.
Wakati ule watu wengi walichomewa moto nyumba zao na kulazimika kwenda kuishi porini na kupoteza mali zao. Visima na maskuli yalitiwa kinyesi na kina fulani ili papatikane visingizio vya kukamata watu.
Baadaye komandoo aliamrisha kuvunjwa nyumba kadha hapo Mtoni Kidatu na wapo waliopoteza maisha yao kwa mshituko wa moyo na ufukara waliotiwa na komandoo kwa sababu za kisiasa. Kinara wa uvunjaji nyumba zile alidaiwa kuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magahribi, Abdulla Rashid.
Watu wengi, hasa wenye asili ya Kisiwa cha Pemba, walifunguliwa kesi bandia za madai ya kuwa wazembe na wazururaji au kumtukana rais. Ilikuwa balaa ya aina yake.
Kwa hakika hali hii si tu kuwa ilikuwa inasikitisha, bali pia ilikuwa ya kutisha. Wakati ule nilisema: Hii ni hali ambayo haipaswi kunyamaziwa kimya na aliyekuwa Inspekta Jenerali wa Polisi, Omar Mahita.
Nilimueleza Mahita, kuwa baadhi ya hao waliopigwa vibaya sana ni maofisa wastaafu wa Jeshi la Polisi ambao wakati ule walikuwa mara kwa mara wakikamatwa na kupigwa panapotokea mtafaruku wa kisiasa Visiwani.
Nilieleza kuwa uzoefu wangu wa kufanya kazi kwa karibu na aliyekuwa Rais Benjamin Mkapa alipokuwa Mhariri Mtendaji wa Daily News ulinipa mashaka kama hali ile ya mateso waliokuwa wanapata Wazanzibari ilikuwa inamsumbua.
Wakati mmoja Mkapa alisema baadhi ya mambo ya Zanzibar yalikuwa yanamkosesha usingizi, lakini nikaeleza wasiwasi wangu kama alikuwa na nia hasa ya kumaliza balaa ile iliyokuwepo wakati ule. Sikushangaa alipomuachia urithi wa maovu yale Rais Jakaya Kikwete mwaka 2000.
Nimeeleza haya hii leo kuonesha wasiwasi wangu kwamba ile hali mbaya ya siku za nyuma huenda ikarudia Zanzibar kama hapatakuwepo ustahamilivu, kuondosha uonevu na kuachana na mtindo wa kubuni kesi bandia.
Panapotokea mzozo sheria iachiwe ichukue mkondo wake na siyo kudhalilisha watu kwa kuwapiga bakora, kuwanyoa ndevu, kuwanyima chakula na haki ya kukoga na kubadili nguo wakati wakiwa mahabusu kama tunavyoona hivi sasa. Jamani tukumbuke Mungu yupo!
Hivi sasa tayari watu wamekuwa na mashaka makubwa na hali iliyopo Zanzibar na baadhi ya nchi zimeshaanza kulalamika juu ya vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu Visiwani.
Sura iliyopo sasa Zanzibar ya serikali ya umoja wa kitaifa ni chafu na inanuka na inahitaji kusafishwa na kufukizwa ubani na udi. Kweli Polisi wanaosema hawahusiki wanashindwa kuwadhibiti hao tunaoambiwa ni vikundi vya Ubaya Ubaya na Mbwa Mwitu?
Au Zanzibar ya leo ina vikundi vya mafia kama tunavyoona katika baadhi ya nchi za Amerika ya Kusini?
Dunia inatuangalia na tayari taasisi za kutetea haki za binadamu kama Amnesty International zinasema hakuna utawala bora Zanzibar.
Mahakama zetu lazima zifanye kazi ya kuonekana kuwa huru na si zinavyoonekana hivi sasa. Hatutaki baadaye kuwasikia mahakimu na majaji wanajikosha kama ilivyofanyika katika miaka ya karibuni kwamba walikuwa wanapelekewa vikaratasi kuelezwa wazishughulikie vipi kesi mbali mbali.
Siasa ni mchezo wa mbinu nyingi za wazi na za siri, lakini huu mchezo mbaya wa kupiga watu majumbani, kuchezea miili yao kwa kuwanyoa ndevu na kuifanya dhamana kama siyo haki ya mshitakiwa ni wa hatari.
Viongozi wakuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Rais Ali Mohamed Shein na Makamu wake wawili, Maalim Seif Sharif Hamad na Balozi Seif Iddi, wajue wao ni dhamana na hawawezi kukwepa dhamana hiyo watakapotakiwa watoe maelezo kwa nini waliruhusu maovu yanayofanyika sasa.
Huu mchezo wa kunyamazia maovu, kama utaachiwa kuendelea, utatoa sura mbaya katika kumbukumbu za historia kama ilivyo kwa iliyokuwa Czechoslovakia, Ethiopia wakati wa utawala wa dikteta Mengistu, Chile wakati wa utawala wa Agostino Pinochet na mauaji ya halaiki yaliotokea Rwanda.
Zanzibar haiwezi kukaribia huko lakini kila jambo lina mwanzo wake . Wakati wa utawala wa komandoo Salmin Amour hali mbaya ilianza kama hivi na baadaye tukashuhudia watu wengi wakipoteza maisha yao na kuwa vilema.
Orodha ya majina ya watu waliouawa, kujeruhiwa na kufungwa jela kwa maonevu inajaza ukurasa huu. Huo ndio ukweli na waliofanya kama hawataki yaelezwe wasingethubutu kutenda maovu yale.
Ni vizuri hatua zikachukuliwa haraka kuzuia hali tete iliyojaa hasama na maonevu yaliopo sasa kudhibitiwa. Moto huanza na cheche na tayari cheche tunaziona na zikiachiliwa watatokea watu kuzimwagia petroli.
Tusingojee moto kupanda juu ya paa na ndipo tukaanza kufanya juhudi za kuuzima. Tukumbuke ule wimbo wa Malindi usemao: Moto ukija kuwaka mzimaji nani?
Wale wenye kupanga njama hizi za maovu na kutaka kuirejesha Zanzibar ilipotoka wasipewe mwanya wa kupumua. Mchezo wao utatuponza sote na kuja kujutia.
Tukumbuke ni rahisi kubomoa kuliko kujenga na wazee walituasa kwa kutuambia….majuto ni mjukuu na tukifanya masihara majuto yetu yanaweza kuwa ya vilembwe na vitukuu.
Tushirikiane kuirejesha Zanzibar katika hali ya utulivu na kama mtu anataka kupiga watu anunue ngoma na apige mpaka ipasuke, si kupiga migongo ya watu na anayetaka kunyoa ndevu anunue beberu na ajifunze kunyoa ndevu na si za watu wengine.

Tuesday 6 November 2012

Tume huru ndiyo itakayoeleza ukweli Z’bar

Na Salim Said Salim
MARA nyingi ninaposomesha waandishi wa habari nawaeleza kuwa kuandika uwongo au kuzua jambo sio vibaya na kwamba hiyo ni haki ya msingi ya kila mtu.
Lakini huo uwongo ukishaandikwa, huyo mwandishi anatakiwa ausome mwenyewe, pia si vibaya kama ataamua kuuamini na sio kuuuchapisha katika gazeti au kuutangaza katika redio au kituo cha televisheni.
Njia nzuri ya kuusoma uzushi huo na kujifurahisha ni kwa huyo mwandishi kufanya hivyo akiwa amejifungia chumbani peke yake.
Kuupeleka katika jamii ni kinyume cha maadili ya taaluma ya habari na ni dhambi.
Ninasikitika kuona baadhi ya wanasiasa, viongozi wa serikali na Jeshi la Polisi wanazua uongo wa dhahir shahir na kuja hadharani kuueleza umma na kuwataka watu wauamini na kuukubali.
Katika miaka yangu ya zaidi 45, nimeshuhudia kauli nyingi za uwongo, zikiwemo zile zisizokuwa na kichwa wala miguu kutoka kwa waandishi wa habari, wana siasa, viongozi wa serikali na hata wa dini.
Ninakumbuka katika utumishi wangu wa karibu miaka 10 kama mjumbe wa Baraza la Habari la Tanzania (MCT), nilishuhudia waandishi wakibuni habari za aina kwa aina na mojawapo ni kusingizia mtu mmoja kuwa kabaka na kupelekwa mahakamani.
Katika habari ile alitajwa kwa jina la mwendesha mashitaka na hakimu aliyesikiliza ile kesi na kumpa dhamana.
Kumbe yote yale yaliyoandikwa baada ya kuyafuatilia yalikuwa ni uzushi uliokuwa na lengo la kumpaka matope yule aliyedaiwa kubaka ambaye alikuwa ana lengo la kugombea udiwani katika eneo la Ubungo, Dar es Salaam.
Uwongo mwingine ambao kama ungeliingizwa katika mashindano ungenyakuwa medali ya dhahabu kama sio ya lulu au almasi ni wa taarifa ya Jeshi la Polisi baada ya polisi kuuwa na kujeruhi wengine kule Pemba katika Kijiji cha Shumba Mjini, Micheweni wakati wakipandisha bendera ya tawi la Chama cha Wananchi (CUF) baada ya mfumo wa vyama vingi kuingia.
Polisi walidai, tena bila ya aibu, kuwa ati risasi zilipigwa hewani. Jamani toka lini risasi iliyopigwa hewani inateremka chini na kuumiza makalio au mgongo wa mtu. Toka siku ile nimekuwa na wasi wasi na kauli zinazotolewa na maafande wa Jeshi la Polisi.
Katika vurugu zilizotokea Zanzibar hivi karibuni na kusababisha viongozi wa Jumuiya ya Uamsho kukamatwa na kunyolewa ndevu hata kabla ya kesi kuhukumiwa, tunasikia kila aina ya uwongo, uzushi na unafiki kila pembe. Kwa kifupi unaweza kusema yapo mashindano Zanzibar ya kudanganya umma.
Watu hawa wananyosheana vidole na wengine kutajana majina ya watu na kuwahukumu utafikiria wao wamepewa kazi ya uhakimu kama ndio waliohusika na vurugu za hivi karibuni.
Kwa maana nyingine, wamejifanya mabingwa wa upelelezi na watu wanapaswa kuwaamini na wasiwahoji.
Hawa ndio wale tunaowaita limbukeni wa siasa kwa sababu wanafikiri siasa ni kusema uongo na kupakazana matope.
Hakuna ubishi kwamba vurugu zimetokea na watu kuuawa na wengine kujeruhiwa. Lakini kuwataka watu wayaone mauaji ya askari polisi, Koplo Said Abdulrahmani, katika eneo la Bububu ndio pekee yaliyotokea sio sahihi na sio haki katika dunia hii na hata mbele ya Mungu.
Roho zote zilizopotea zina thamani sawa na anayeelewa ni roho gani ilikuwa bora zaidi ni mwenyewe aliyetuumba.
Mauaji yote yanapaswa kulaaniwa na sio ya Polisi tu kwani haikuandikwa kwenye msahafu kwamba askari ni kiumbe kitukufu na wengine ni viumbe dhaifu.
Mauji ni mauaji na yote yanapaswa kulaaniwa, yawe ya askari, mfanyabiashara, mchunga ng’ombe au mfuga kuku au mvuvi.
Yote lazima yachunguzwe na wahusika (sio waliosingiziwa) wafikishwe mbele ya vyombo ya sheria.
Jeshi la Polisi na wanasiasa wa chama tawala wa CCM wanalaani mauaji ya askari tu. Wapi imeandikwa katika Kuran au Biblia kwamba akiuawa afande ndio mauaji na akiuawa mtu mwingine ni sadaka?
Zipo shutuma nyingi. Wapo wanaodai kuwa wafuasi wa uamsho wanahusika na mauaji na hata kuvunja maduka ya pombe na kulewa na wapo wanaosema vyombo vya dola vilisababisha vurugu.
Baadhi ya viongozi wa CCM wamewanyooshea vidole viongozi wa chama cha CUF kuwa chanzo cha vurugu na CUF wanadai waliosababisha maafa na wizi ni Janjaweed ambao chama hicho kinadai ni watoto wa CCM.
Lakini pia, zimesikika kauli, tena zenye nguvu, zinazotaja kuwepo kwa makundi yanayojiita Ubaya Ubaya, Mbwa Mwitu, Nguruwe na kadhalika kuwa ndio waliofanya vurugu na hata kuua.
Hapa unajiuliza ukweli hasa ni upi? Nani anasema kweli na nani anasema uwongo.
Njia pekee ni kufanya uchunguzi, lakini kwa kuwa Jeshi la Polisi nalo linanyooshewa vidole, basi njia pekee ni kuwa na uchunguzi wa tume huru. Inawezekana, japokuwa ni tabu kuamini, kuwa polisi wanaweza kufanya uchunguzi wa haki kutokana na tayari makamanda wao kuwashutumu uamsho moja kwa moja huku wakisema upelelezi unaendelea na haujakamilika.
Kama polisi hawajakamilisha uchunguzi inakuwaje leo wawalaumu uamsho?
CUF nao wanasema hawa vijana wanaodaiwa kuhusika na vurugu ni wale wanaowaita Janjaaweed ambao CUF inadai walikusanywa na CCM kwa ajili ya kufanya ghasia na kupiga kura mara mbili mbili katika uchaguzi na kutokana na kukosa ajira sasa wameamua kufanya uhalifu.
Sijui CUF wamepata wapi uthibitisho huo wa kukinyooshea CCM kidole cha lawama.
Lakini lililo baya zaidi ni hizi hukumu zinazotolewa. Sijuwi kwa nini polisi haitaki kuiachia mahakama kuhukumu au ndiyo tuseme kazi hiyo sasa wamekabidhiwa wao?
Nimesema na ninarudia kwamba ni tume huru tu, tena ile itakayopata imani ya wananchi, ndiyo inaweza kutoa jawabu na si vinginevyo.
Hawa vijana wa Ubaya Ubaya wamekuwa wakilaumiwa muda mrefu kwa vitendo vya uhalifu kabla ya vurugu za hivi karibuni, lakini wamekuwa wakiendeleza ubaya wao kama vile wamepewe leseni ya kufanya hivyo. Inasikitisha, tena sana.
Kama kweli Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambayo viongozi wake sasa wanaonekana kugawanyika mapande mawili, moja la CCM na jingine la CUF, linataka kutafuta ukweli basi iundwe tume huru ya uchunguzi.
Si vibaya hata kama wajumbe wa tume hiyo watatoka Tanzania Bara au katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na si Zanzibar ambapo inaonekana utashi wa kisiasa, uongo, unafiki na uzandiki unatumika kufunika ukweli.
Kama hawa waongo, wanafiki na wazandiki wanafanya haya wakiwa ndani ya majumba yao ni sawa, lakini wanapeleka uovu wao huu hadharani na kutaka watu wauamini.
Watu wa Zanzibar sio mbumbumbu kama hao wazushi, waongo na wanafiki. Wanaujua ukweli na siku zote ukweli haufichiki, hasa katika zama hizi za ukweli na uwazi.
Wapo watu waliopiga picha na kuchukuwa video na wapo wanaodai kuona yaliyotendeka. Kinachongojewa ni nafasi ya kuyaweka hadharani. Kama hapana hofu ya ukweli kujulikana kwa nini serikali iwe inaona vigumu kuunda tume huru ya uchunguzi?
Tume hii pia itafute ukweli juu ya hao wanaoitwa Janjaweed. Je, kweli wapo watu hawa? Nani aliwakusanya, waliwekwa wapi, nani aliwahudumia na kama walikuwepo nini yalikuwa makusio ya kuunda kikosi hiki?
Yapo maeneo ambayo yanadaiwa ndipo walipowekwa na wanadaiwa kwamba vijana hawa walitumika katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Bububu uliofanyika karibuni.
Kwa kweli shutuma zinazosikika ni ndefu na jawabu ni kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi. Kutoifanya hivyo hakutatoa tafsiri yoyote ile isipokuwa kutaka kuficha ukweli.
Hatukatai kuwa kazi ya kutafuta wahalifu imekabidhiwa Jeshi la Polisi, lakini lazima tukumbushane kwamba hawa maafande sio manabii au malaika na upo ushahidi kwamba polisi katika nchi nyingi wamekuwa wakitoa taarifa za uongo.
Mfano mmoja tu wa hivi karibuni ni namna ambavyo Jeshi la Polisi la Uingereza lilivyofanya uubunifu wa kuwasingizia mashabiki wa timu ya Liverpool kuwa ndio waliofdanya vurugu zilisababisha vifo vya watu wengi katika uwanja wa mpira.
Baada ya miaka 19 ya uongo wa Jeshi la Polisi ukweli umepatikana na sasa wanaohusika wanawajibishwa kisheria, Au na sisi tunangojea itimie miaka 20 ndio tuungojee ukweli?
Jaribio lolote la kuficha ukweli linaweza kuvumiliwa leo na kesho, lakini ipo siku watatokea watu wataifichua kama ilivyofanyika kwa uwongo wa polisi wa Uingereza.
Wazanzibari au Watanzania kwa jumla wanataka kuujuwa ukweli na nafasi nzuri ya kutimiza kiu yao ni kuiachia tume huru kuifanya kazi hiyo.
Katika makala yangu ya hivi karibuni niliuliza; Zanzibar inaelekea wapi?
Sasa nimeipata ishara zinazonipa hisia za jawabu ya suala langu. Nazo ni kwamba visiwa hivi vinarudia kule tulikotoka ambapo siasa za mvutano, unafiki na uzandiki zilitawala na kusabaisha watu kuuawa na wengine kuwa vilema.
Kama siasa hizi zitaachiwa basi yale maridhiano ya kisiasa yalioleta umoja wa Wazanzibari na kusababisha kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa yatakuwa hayana maana wala faida tena kwa Wazanzibari.
Wanaohusika wasije kusema wanaonewa wakihukumiwa kwa haya maovu wanayoyatenda hivi sasa.
Wenzao katika nchi mbali mbali walijifanya majabari, walitukana watu ovyo pembezoni na hadharani na wakapika majungu ya uovu na kuacha wengine kuyapakua.
Leo wanatiwa kamba ya shingo, wanalia na kutaka wahurumiwe. Ninawakumbusha kuwa sheria haina huruma, kwani humhurumia asiyetenda kosa na humuadhibu anayetenda maovu.
Tanzania Daima

Thursday 1 November 2012

Indhari kwa watawala na watawaliwa Zanzibar

ALBIUS Tribullus alifariki dunia kama miaka 19 hivi kabla ya kuzaliwa Nabii Issa (YesuKritso). Tribullus alikuwa Mlatini na mshairi maarufu aliyebobea katika fani ya uandishi wa maombolezi.
Mshairi huyu wa huba na huzuni aliwahi kuandika: “Matumaini daima hutwambia kwamba kesho mambo yatakuwa mazuri zaidi.” Matumaini kama hayo wanayo Wazanzibari wa leo. Yanawaambia kesho mambo yatakuwa mema zaidi lakini kwa sharti.
Sharti lenyewe ni kwamba wajichunge. Watawala na watawaliwa; wale wenye silaha nzito nzito na wale wenye mawe na vibiriti wote wajichunge na wajifunze kutoka historia.
Historia ya kisiasa ya Zanzibar inaonyesha kwamba kwa kipindi cha zaidi ya miongo mitano, tuseme tangu zilipoanza siasa za vyama mwaka 1957 visiwa hivi vimeshuhudia visa vingi vya vurugu, umwagaji wa damu, kuteswa kwa raia na kuuawa kwa mamia ya watu.
Kuna raia walioteswa na waliolemazwa au waliofanyiwa mambo hata akili zao zikaharibika. Hawakuathirika wao tu bali hata familia zao na jamii nzima kwa jumla.
Vitendo hivyo vya kinyama na kikatili viliwezekana kwa sababu watu hawakuweza kuvumiliana kisiasa. Kwa kawaida visa kama hivyo havitokei katika jamii zilizostaarabika ambako watu wenye maoni au itikadi tofauti za kisiasa hupambana kwa njia za amani. Wanapambana kwa mujibu wa kanuni za kidemokrasia, za utawala bora na kwa kuzifuata sheria za nchi.
Bahati nzuri hii leo Zanzibar juu ya vurugu za kusikitisha zilizotokea Unguja majuzi bado kuna hali ya amani na utulivu wa kisiasa. Si hayo tu bali wengi wa Wazanzibari wanataka hali hii ya amani iendelee na matatizo yote ya kisiasa ya tanzuliwe bila ya umwagaji damu, machafuko ya raia au hatua yoyote itakayozua balaa.
Lengo lao ni kuvifanya visiwa hivi viendelee kuwa visiwa vya amani. Hayo ndiyo matakwa ya wananchi. Ninaamini kuwa hayo pia ni matakwa ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Ni muhimu lakini serikali ionyeshe kwamba inakubaliana na wananchi wake kuwa matatizo yote yatanzuliwe kwa kufuata sheria za nchi.
Kama kuna watu wenye kushutumiwa kwa kufanya mambo yasiyokubalika au wanaoshutumiwa kwa vitendo vya uhalifu basi lazima wahakikishiwe na wapewe haki zao zote za kikatiba wanaposhikwa na vyombo vya dola. Yasipofanyika hayo basi hivyo vyombo vya dola na hatimaye serikali yenyewe ndio wanaokuwa wahalifu wa sheria.
Jamii zilizoendelea kimaadili kwa kawaida huwapa wananchi wao haki za kimsingi za binadamu zikiwa pamoja na uhuru wa kusema, uhuru wa kukusanyika na wakujiunga na jumuiya yoyote waitakayo. Visiwani Zanzibar haki zote hizi zipo kwenye katiba lakini hazijatolewa tu hivi hivi na serikali. Zilipiganiwa na Wazanzibari wengi. Kuna baadhi yao walioyasabilia na kuyatolea mhanga maisha yao kwa nchi yao na watu wake wote.
Katika mazingira ya sasa ya Zanzibar lazima pawepo na amani endelevu na ilikuipata amani aina hiyo panahitajika utamaduni uliokomaa wa kuvumiliana kisiasa pamoja na siasa za ukinzani wa amani.
Hizi ni sifa muhimu za kuukuza mfumo wa kidemokrasia. Na hapa tunautafsiri mfumo huo kuwa ni ule wenye kusababisha kupatikana kwa maridhiano juu ya mambo kadhaa ya kimsingi kama vile kwa mfano kutokiukwa kwa uhuru wa nchi, umoja wa watu wake na msimamo wao wa kuiunga mkono serikali yao inapotetea maslahi ya nchi yao.
Ninavyohisi ni kwamba utaratibu huu wa amani na wa pande zote kuweza kukaa pamoja na kubadilishana mawazo ndio suluhisho pekee kwa matatizo yote ya kisiasa yanayoikabili Zanzibar ya leo. Na kwa hakika tukiyaangazia masuala makuu yanayoikabili Zanzibar hii leo, tunaona kwamba suala kubwa kabisa linalowashughulisha wengi ni lile la mchakato unaoendelea wa kulitafutia taifa katiba mpya. Kuna haja kubwa ya kuhakikisha kwamba mengine yanayotokea kwenye ukingo wa medani ya siasa, ingawa yanaudhi, yasiubabaishe umma na kuufanya upoteze dira.
Hivyo ni muhimu kwamba pawepo busara na watu wajizuie kuongozwa na hamasa zao. Agizo hili ni muhimu hasa kwa viongozi wote wa kisiasa, viongozi ambao lazima wakate maamuzi yao kwa kulingana na mahitaji ya halisi ilivyo ili ule msingi wa ‘nguvu ya hoja’ na siyo ‘hoja ya nguvu’ uwe ndio wenye kuongoza mahusiano baina ya Wazanzibari na baina yao na serikali yao.
Hatutoweza kuiendeleza demokrasia endapo hatutambui kwamba ‘serikali ya kidemokrasia’ inadhamana ya, na inawajibika kwa, watu wote. Inatupasa pia tutambue kwamba serikali aina hiyo haipaswi kuwabagua wale waliovipigia kura vyama vingine na wala haipaswi kuvihodhi vyombo vya dola au idara ya utumishi wa serikali kwa sababu za kiitikadi.
Iwapo serikali itayafanya hayo isiyopaswa kuyafanya basi itawanyima haki za kiraia na kuwatenga wale wasionufaika na fadhila za utawala.
Katika hali nyeti inayoibuka sasa Zanzibar kuna umuhimu kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kuonekana kwamba inafanya kazi pamoja kwa ushikirikiano wa wabia wake wote katika kuendesha shughuli za nchi. Serikali sharti iwaonyeshe wananchi wake kwamba sera zake zote zinakubaliwa na wabia wote wawili katika serikali hiyo (yaani chama cha CCM na kile cha CUF) na kwamba wote wanachukua dhima ya pamoja kuhusu maamuzi yote ya serikali. Hiyo ndiyo njia ya pekee ya kuhakikisha kwamba pataendelea kuwako umoja, amani na utulivu wa kisiasa katika nchi yetu.
Raia Mwema